Wakili asema kifo cha George Floyd kilipangwa.

Wakili wa familia ya George Floyd, ambaye kifo
chake kiliibua maandamano ya hasira kote nchini Marekani , amemshutumu afisa wa
polisi kwa “kupanga mauaji”.

Polisi wa Minneapolis Derek Chauvin ameshitakiwa
kwa mauaji , lakini wakili Benjamin Crump amekiambia kituo cha habari cha CBS
news kuwa yalikuwa ni mauaji ya kiwango cha kwanza.


“Tunadhani kwamba alikua na nia … takriban
dakika tisa aliendelea kushindilia goti lake kwenye shingo ya mwanaume ambaye
alikua anamuomba amsamehe na kumwambia kuwa hawezi kupumua,” alisema

matukio ya uporaji yameripotiwa katika jimbo la
Philadelphia.

Video kutoka katika vituo viwili vya televisheni
vya Philadelphia Jumapili zilionesha vijana wakivunja magari kadhaa ya polisi
na kuiba katika duka moja .

Rais Donald Trump alituma ujumbe wake wa twitter
uliosema: Sheria na amri vifuatwe Philadelphia, SASA! Wanapora maduka. Walete
wanajeshi wetu waingilie kati “.

Tukio la Floyd limeibua ghadhabu miongoni mwa
Wamarekani juu ya mauaji yanayotekelezwa na polisi dhidi ya watu weusi.

Hii inafuatia kesi maarufu ya mauaji ya Michael
Brown mjini Ferguson, Eric Garner mjini New York na kesi nyingine
zilizowasilishwa mahakamani na vuguvugu linalojulikana kama Black Lives
Matters.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )