Wagombea CCM Stop kutumia matarumbeta, watakiwa kuchukua fomu kimya kimya

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey
Polepole, amesema kuwa wagombea wa nafasi mbalimbali katika uchaguzi ujao,
hawapaswi kutumia matarumbeta wakati wanaenda kuchukua fomu za ugombea, badala
yake waende kimya kimya na matarumbeta yatapigwa mara baada ya chama kumteua
mgombea.

Polepole ameyabainisha hayo leo Juni 2, 2020,
wakati wa uzinduzi wa kituo maalum cha wananchi kutoa taarifa za uchaguzi
kimaadili ili kuwabaini wala na watoa Rushwa katika kipindi cha kuelekea kwenye
Uchaguzi Mkuu Oktoba, 2020.


“Mchakato utaanza baada ya kuwatangazia na
ndiyo kwa unyenyekevu na siyo kwa mbwembwe, utakwenda taratibu na si kwa
matarumbeta kwenye ofisi ya chama kupata fomu yako, ukiipata kaijaze kwa
umakini na kuirejesha, tarumbeta zitakuja baada ya kupata mtu mmoja hodari
atakayeiwakilisha CCM kwenye uchaguzi” amesema Polepole.

Aidha Polepole ametoa rai kwa wananchi kwamba,
wasidanganyike na wale watu wanaopita katika maeneo yao kujitangaza kwamba
wameagizwa na Mwenyekiti wa chama kugombea, kwa kuwa ni walaghai na
wasiwasikilize kwani hakuna mtu aliyeagizwa kufanya hivyo.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )