WAFANYABIASHARA WA VITUNGUU SINGIDA WAHAKIKISHIWA USALAMA WA MALI ZAO.

Mwenyekiti  wa Soko la Kimatifa la  Vitunguu Mkoa wa Singida, Iddy Mwanja
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)


Vitungu vikiwa vimeanikwa katika Soko la Kimatifa la  mkoani Singida.

Vitunguu vikianikwa katika soko hilo.

Vitunguu vikianikwa katika soko hilo.
 Na Ismail Luhamb, Singida

Wafanya biashara wa vitunguu Mkoani Singida wamehakikishiwa usalama wa mali zao katika msimu wa mwaka 2021.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti  wa Soko la Kimatifa la  vitunguu Iddy Mwanja,lililopo  Kata ya Misuna mkoni Singinda baada ya kukutana na Waandishi wa habari ofisini kwake na kueleza kufunguliwa rasmi soko hilo siku chache zijazo.

Akifafanua Mwenyekiti Amesema mwaka huu wamejipanga vizuri kuliko misimu yote ya nyuma na kila kitu kipo sawa kwa sasa kuanza kupokea Bidhaa ya vitunguu kutoka kwa wakulima mbali mbali ndani na nje ya Tanzania..

Ameendelea kusema  wao Kama Viongozi wa soko hilo wamejipanga kila sekta, japo kuna changamoto mbali mbali zinazo likabili soko hilo moja ya changamoto ni madimbwi au mashimo yaliopo kwenye hili soko na uchafu kwenye dampo na tope.

“Hapa mvua ikinyesha hakuna hata sehemu ya kukimbilia zaidi ya kwenda kumwaga vitunguu kwenye nyumba za watu.” alisema Mwenyekiti

“Lakini hata hivyo tumewasilina na mamlaka za Serikali yetu ya Mkoa wamehaindi kufanya ukarabati wa soko kabala ya Tareh Moja ambo tunatengemea kufunguwa msimu mpya wa kuuza bidha za vitungu.”
Kwa sasa tunapima gunia kilo 100 mpaka 120 na mwaka huu tumeruhusu net za Mangufuli zenye ujazo wa kilo 85 mpaka 100, na ole wao tutakaowakuta na net za shishimbi tutawafukuza au tutawachukulia hatua kali za kisheria.


Mwanja aliwakaribisha wakulima wote kuleta vitunguu vyao hapo ambapo watauza kwa amani kabisa na watapata faida ya kilimo chao kwani hilo soko watu kutoka mataifa mbalimbali wanakuja hapo kununua vitunguu na kuvipeleka kwenye nchi zao
CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )