Waendesha Bodaboda na Bajaj wampongeza Rais Magufuli kwa Corona

CHAMA cha Waendesha Bodaboda na
Bajaj- Taifa kimempongeza Rais John Magufuli kwa namna alivyoshughulikia
ugonjwa wa Covid-19 unaoambukizwa na virusi vya corona akiruhusu
shughuli za kiuchumi na kijamii kuendelea.

Mwenyekiti wa chama hicho, Edward Mwenyisongola amesema uamuzi huo
umekuwa wenye tija kwa waendesha bodaboda na bajaji kwani umewawezesha
kuzitumikia familia zao.

Amesema shughuli zisingeruhusiwa kuendelea kama kawaida, wananchi
wangekufa kwa njaa huku vitendo vya uhalifu pia vikiongezeka. Amesema
waendesha bodaboda wanatoa pongezi na wataendelea kufanya kazi na
serikali huku wakitii sheria na kanuni za usalama barabarani.

“Waendesha bodaboda na bajaji tunamshukuru Rais Magufuli na serikali
kwa uamuzi wa haki, weledi na uliozingatia maisha ya Watanzania kwa
kuruhusu shughuli kuendelea,” amesema.
CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )