WACHIMBAJI WA MADINI WATAKIWA KUFUATA MCHAKATO WA UCHIMBAJI MADINI WA WAZI

Na,Jusline Marco;Simanjiro

Waziri wa madini Dotto Biteko amewataka  wachimbaji wa madini kujiunga na mchakato wa uchimbaji madini wa uwazi ili kuweza kunufaika na madini hayo.

Akizungumza wakati wa hafla ya kupokea jiwe la Tanzanite lenye uzito wa kilo 6.33 ambalo limenunuliwa serikali kwa shilingi  bilioni 4.846 kutoka kwa mchimbaji mdogo wa madini,Saniniu Laizer iliyofanyika katika viwanja vya Mirerani Mkoani Manyara.

Aidha ameongeza kuwa serikali haitakubali kuona mchimaji wa madini  anayechimba kwa haki hataonewa na mtu yeyote ambapo amesema baada ya kupatikana kwa madini hayo kupatikana wizara inayokazi ya kuhakikisha uongezaji thamani wa madini unafanyika hapa nchini.

Kwa upande wake waziri wa fedha na mipango Dkt.Philip Mpango amewataka wachimbaji hao kuwa na uzalendo kwa nchi yao kwa kupambana na umaskini wa eatu wengine huku wakihakikisha madini hayo hayanufaishi watu wengine.

Awali akizungumza katika hafla hiyo Naibu Waziri wa madini Mhe.Stanslaus Nyongo   ameseme kuwa kwa mwaka 2020 sekta ya madini imeongezeka kwa asilimia 17.7 na imezidi kukua na kuweka mchango mkubwa katika uchumi wa nchi kwa asilimia 5.2 kutoka asilimia 3.8.

Pamoja na hayo Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini,Jenerali Venance Mabeyo amesema kuwa mafanikio yanayoshudiwa katika sekta ya madini ni matokeo ya juhudi kubwa za wizara husika na serikali ya awamu ya tano katika kuboresha sekta ya madini kwa lengo la kuhakikisha kuwa sekta hiyo inawanufaisha watanzania.

Ameongeza kuwa hatua hizo ni pamoja na kufanya marekebisho ya sheria na mikataba mbalimbali ya madini pamoja na ujengaji wa ukuta ili kudhibiti utotoshaji wa madiji uliokuwa ukifanywa na baadhi ya watu wasio wazelendo.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )