UVCCM RUVUMA WATEMBELEA MIRADI YA JUMUIYA HIYO

Kamati ya Utekelezaji ya Uvccm Mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na Mwenyekiti  Comredi Raymund Gerold Mhenga Imeendelea na ziara yake Wilaya ya Namtumbo kwa Mwenyekiti kuzindua Baraza la Vijana la Wilaya ambapo alipata fursa ya kuzungumza na Vijana kuhusu umuhimu wa kuwa wamoja hasa kipindi hiki cha uchaguzi na kuhakikisha wanatafuta kura za CCM hili kuhakikisha CCM inashinda kwa Kishindo.

Mwenyekiti aliwaeleza Vijana kazi nzuri ya Utekelezaji wa Ilani iliyofanywa na Rais wetu Dr Joh Pombe Magufuli Kitaifa na kwenye Mkoa wa Ruvuma na Wilaya ya Namtumbo na kuwataka Vijana kuhakikisha wanawaeleza Vijana wengine mambo hayo.

Pia Kupitia Baraza hilo Mwenyekiti Raymund Mhenga kwa niaba ya Vijana wote wa Mkoa wa Ruvuma alimpongeza Rais Dr John Pombe Magufuli kwa namna alivyoshughulikia janga la Corona kwa uthabiti wa hali ya juu bila kupelekwa na ushawishi wa mataifa ya Magharibi.

Kamati ya utekelezaji ilitembelea Mradi wa uwezeshwaji vijana chini ya ofisi ya Waziri mkuu wa Kitalu Nyumba,Vikundi mbalimbali vilivyowezeshwa na Mkopo wa Vijana wa asilimia 4% sambamba na kujionea eneo la Uvccm ambalo wamepanga kuanza ujenzi wa Nyumba ya Katibu wa wilaya pamoja na Fremu za Biashara.Mwenyekiti alishukuru serikali ya Wilaya ya Namtumbo kwa kuwezesha Vijana kupatiwa eneo hilo.

Imetolewa na katibu Hamasa na Chipukizi
Twaha Saanane Mchata

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )