Uvccm Arusha waridhishwa na utekelezaji wa Ilani Karatu

 

Mwenyekiti  wa Uvccm Mkoa wa Arusha Omary Lumato aridhishwa na utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi 2015 katika Tarafa ya Mbulumbulu Wilayani Karatu Mkoani Arusha  katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  iliyowasilishwa na Afisa Tarafa huyo Saitoti  Zelothe.

Akizungumza katika hafla Ndugu Lumato amewataka vijana wa Mkoa wa Arusha kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu unaofanyika Oktoba  na kuwasihi kuacha kutumika katika makundi bali wajitokeze kukisaidia chama ili kiwezwe kushinda uchaguzi mkuu kwa kishindo.


Nipende kuchukua fursa hii kumpongeza Mwenyekiti wetu wa Chama cha Mapinduzi Taifa na Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli “Ameonyesha uwezo wake na weledi wake katika kupambana na janga hili la maambukizi ya homa ya mapafu  (Corona) kwani hakuweka “LockDown” wala kufunga mipaka ila aliwasihi watanzania kufuata taratibu zote zilizokuwa zinatolewa na wataalamu wa afya na sasa tunaona mataifa mbalimbali duniani wameamua kufuata nyayo za Rais wetu magufuli kwa hili ametutendea vyema sisi wananchi wanyonge” 

“Hongera sana Ndugu yangu Saitoti Zelothe Afisa Tarafa wa mbulumbulu kwa kuwa Afisa Tarafa wa kwanza Tanzania hii kwa kusoma uwasilishwaji wa Ilani ya chama umekuwa mfano kwa wenzako niwatake maafisa tarafa wengine mkoa huu kujitokeza na kufanya kama wewe pia hongera kwa  kwa kazi kubwa ya kuwatumikia wananchi kwa moyo mmoja”


“Vyote vilivyowasilishwa hapa tumejionea uadilifu, Uwajibikaji,uzalendo na uchapaji kazi wa viongozi wa Serikali uliopelekea kufanya vyema utekelezaji wa ilani ya uchaguzi. Chama cha Mapinduzi  kupitia Jumuiya yetu ya Umoja wa Vijana  tumeridhishwa na maendeleo mnayoendelea kuwaletea wana Mbulumbulu hawa.Nawapongeza sana kwa kazi kubwa na nzuri ya utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo.”

Akizungumza mara baada ya kumalizika ziara hiyo, Afisa Tarafa hiyo Saitoti  Zelothe amewashukuru viongozi waote wa Chama cha Mpainduzi mkoa wa Arusha kwa kutambua juhudi kubwa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi waliyoiona. Saitoti amemuhakikishia ushirikiano mwema Mwenyekiti wa Uvccm kuwa  katika kuhakikisha yote yaliyohaidiwa na Mhe. Rais Magufuli yanatekelezwa ndani ya Tarafa ya Mbulumbulu.CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )