Utafiti wathibitisha wanaume walioambukizwa Corona kuwa tasaRipoti mpya kutoka Wizara ya Afya nchini Urusi imethibitisha kuwa, maambukizi ya virusi vya Corona (Covid-19) yamebainika kuwa chanzo cha kupunguza ubora wa mbegu za kiume na vinasababisha wanaume kuwa tasa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la RT, matokeo hayo yanatokana na utafiti wa kisayansi uliofanywa na wataalam wabobezi katika masuala ya afya nchini humo.
“Leo, matatizo ya utasa hususani utasa kwa wanaume unaotokana na maambukizi ya Covid-19 yanajidhihirisha kwa kiwango kikubwa, “anasema Elena Uvarova ambaye ni Mtaalam Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watoto na Vijana katika Wizara ya Afya ya Urusi.

Ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari mjini Moscow kupitia mkutano wa kutoa tathimini ya kile ripoti imeainisha juu ya matokeo hayo ya utasa kwa wanaume.
Uvarova amesema kuwa, utafiti umebainisha kuwa, kuna upungufu wa asilimia 38 katika viwango vya ubora wa manii kwa wanaume waliopona virusi vya Corona.
“Huu ni ugunduzi ambao unatoa tafakari ya kina ya juu ya nini kifanyike,kwani ubora wa jumla wa manii kwa wanaume wa Urusi tayari haukuwa kamili,”ameongeza.

Watafiti wamekuwa wakijadili juu ya athari inayowezekana ya Covid-19 juu ya uzazi wa wanaume tangu janga hilo lilipoanza huko Wuhan nchini China mwezi Desemba, 2019.
Baadhi ya tafiti zinabainisha kuwa, virusi viliathiri mfumo wa uzazi wa kiume na huenda ukaathiri kabisa mfumo huo hivyo kuchangia wanaume wengi kuwa tasa.

Source : Majira
CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )