USHAURI WANGU KWA WABUNGE WENZANGU WOTE NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI

DR GODWIN.O.MOLLEL MBUNGE SIHA

       NO. 0764594078

Kwanza nianze kwa kuipongeza serikali kwa jinsi inavyo pambana  vizuri na tatizo hili la Corona,

Kupambana na ugonjwa Kama huu haina tofauti na kupigana  vita ,na vita yoyote haitaji  wasemaji  wengi inaitaji wasemaji wa chache wenye ujuzi wa Kutosha kusemea vita, au wenyekusema baada ya ushauri wa Kutosha na kina kutoka kwa WATAALAMU  waliobobea kupigana vita.

Na HATA Kama wewe ni mtaalamu  wa vita ,Na siyo mamlaka ya kusema ,ukiwa unajambo unataka kushauri shauri kupitia mifumo halali  ya WATAALAMU  wa KIVITA ,

Ninaposhauri hivi simaanishi watu wasijadili wala wasiseme  lolote la hasha  na maanishi ,kabla ya kusema au kushauri angalia je ninachosema kimantiki kinaweza  kuchanganya au kuleta taaruki au kifanye  mifumo sahihi ya taarifa iyanze  kutiliwa  mashaka.

Mifumo sahihi ikitiliwa mashaka kwa uzembe wetu na UJUAJI wetu hakika hatawewe hutabaki salama, MIFUMO YA NCHI HII YA AFYA INAFANYA KAZI VIZURI SANA NA SHIRIKA LA AFYA DUNIA(WHO) PIA  NA VYOMBO VIKUBWA VYA SCIENCE  DUNIANI
JE WEWE NI NANI KUHOJI SANA NA KULETA TAARUKI ISIYO YA LAZIMA?

TUSIRUHUSU KAMWE MFUMO HALALI WA NCHI WAKUTOA TAARIFA UKAANZA KUTILIWA SHAKA, KWAAJILI YA MATAMKO YA BAADHI YETU YASIYOPIMWA ,MFUMO WETU UKIANZA KUTILIWA MASHAKA,

1.Mathara  ni makubwa kwetu sisi humu na nchi ,kwani tutapoteza tumaini

2.Tutaufanya mfumo wetu upoteze  kujiamini na ushusha uwezo kitendaji

USHAURI

1.Tupime sana ni yapi  ya kusema mtandaoni na ni yapi ya kumpigia waziri au Wataamu wa  wizara moja kwa moja

2.Tujue vita ikiwa vita siyo siasa tena ni science  kazi yetu ni kumshauri mwenye mamlaka ili tushinde,

3.Tusiruhusu hawa ambao wanafanya kutoa ushauri  publically  tena wao si WATAALAMU ukiwatizama kwa jicho  la tatu utaona tu nikama  vile anatamani  iwe mbaya ionekane alishauri  alikuwa nabii akusikilizwa.

4.Tuwache kutoa matamko kwenye vyombo vya habari kwa kutumia hadidu rejea (fact) za mitaandao usiyo na hakika kuwa chanzo ni vyombo vya kisayansi halali(certified scientific  document)

MSHANGAO KWANGU
1 .Ninashindwa kuelewa inakuwaje mbunge ambaye anakaa mita chache toka kiti cha waziri wa afya ,tena akiwa ndani  ya  bunge ,akiwa na dukuduku YEYE anaona tweeter  ndio pakupeleka dukuduku.

2. Ivi tumesahau  mbunge wewe ni mamlaka tosha wananchi wakisikia unawasiwasi ujarizika ,unadukuduku kimsingi wao wao watapoteza mwelekeo na kukata  tamaa na HATA kinga ya mwili kushuka

3. Vita yoyote ni kwa vitendo na KUAKIKISHA  saikologia (physicology) ya WATU wako na JESHI lako iko sawa,kutaaruki siyo suluhisho kwani tayari uko vitani ,ukipanic usipaniki vina iko palepale.

HITIMISHO

Matatizo  MENGI  ya afya duniani yametatulika kwa kutumia cultural sensitive  approach (kutumia mbinu mwafaka kulingana na mila ,utamaduni imani na HATA uchumi wa eneo husika)  na pia kwa kutumia WATAALAMU na watu walio fundishwa kupeleka ujumbe mahususi uliopimwa unaeleweka bila kuleta maana tofauti kwa JAMII husika.

ELEWA HATAMANENO HUPIMWA,KULINGANA NA MILA ,TAMADUNI,ELIMU,IMANI NA HATA UWEZO WA KIUCHUMI ,TUJIULIZE TUMETAMKA MANGAPI YASIYO PIMWA JE JAMII IMEPATA UJUMBE KAMA ULIVYOTEGEMEWA
JE NANI ATAPONYA TAARUKI?

TUUNGANE HII NI VITA SII JUKWAA LA KUTAFUTA MCHAWI
 KUMBUKA  GONJWA HILI LIMEPIGA WABABE WA SCIENCE WANYE SUPER COMPUTING SYSTEMS ZA VIRUS ,IMEPIGA JUMBA LA KIFALME ,

MKOMBOZI WETU  NI MUNGU UMOJA WETU NA TAFAKURI YA KINA YENYE MISINGI YA SCIENCE KINA,NAUWEZO WA KUFIKIRI KATIKA HALI YA UTUPU(THINKING BEYOND THE BRAIN) NA UTUPU(ROHO) MUNGU NDIO MSINGI WAKE.

ASANTENI
Siyo msaafu ni tafakuri ya kibinadamu
  Dr Godwin Mollel mbunge siha

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )