Tuwe wajanja tusije tukafa kwa kukosa maarifa, mtu akikupa barakoa kataa mwambie akavae na mkewe- JPM

“Watu watakuja Kuwaambia Mvae, Watanzania
tujifunze kuelewa. Anapokuletea Mtu Barakoa na haujui hata ameitoa wapi kataa
mwambie akavae yeye na mke wake na watoto wake Nyumbani kwake TUTAUMIZWA

Tuwe wajanja tusije tukafa kwa kukosa
maarifa” – Rais MAGUFULI


“Ukitaka kuvaa barakoa kashone yako, mbona ni
rahisi tu, barakoa mbona imekaa kama titi moja la Mtu mmoja hivi limekatwa
upande mmoja, weka huku kama… aaah samahani Mh.Waziri nimesema hapa, nilikuwa
nachomekea tu kidogo” -JPM

“Juzi nilikuwa nasikiliza taarifa ya habari kuna
group linaitwa Magufuli Forum wala silijui, ila sishangai Mtu kujiita Magufuli
hata akijiita fisi ni hiyari yake, lakini walikuwa wanagawa barakoa wala
hazijulikani zinatoka wapi, tutaumia kwa kukosa maarifa”-JPM

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )