TUME YA USHIRIKA YAFANYA KIKAO CHA PAMOJA NA TAKUKURUMkurugenzi
Mkuu wa TAKUKURU ,Brigedia Jenerali John Mbungo (kulia) akizungumza
katika kikao cha pamoja kati ya TCDC na Taasisi ya kuzuia na Kupambana
na Rushwa wenye lengo la kuimarisha usimamizi na Maendeleo ya Vyama vya
Ushirika nchini.

Mrajis
wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika
Dkt.Benson Ndiege akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya TCDC na
Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa wenye lengo la kuimarisha
usimamizi na Maendeleo ya Vyama vya Ushirika nchini.

Naibu
Mrajis wa Vyama vya Ushirika,Charles Malunde akizungumza katika kikao
cha pamoja kati ya TCDC na Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa
wenye lengo la kuimarisha usimamizi na Maendeleo ya Vyama vya Ushirika
nchini.

Viongozi
wa tcdc wakiwa katika katika kikao cha pamoja kati ya TCDC na Taasisi
ya kuzuia na Kupambana na Rushwa wenye lengo la kuimarisha usimamizi na
Maendeleo ya Vyama vya Ushirika nchini.

Viongozi
wa TCDC na TAKUKURU wakiwa katika Picha ya Pamoja mara baada ya kikao
cha pamoja kati ya TCDC na Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa
wenye lengo la kuimarisha usimamizi na Maendeleo ya Vyama vya Ushirika
nchini.

Tume ya Maendeleo Ushirika Tanzania (TCDC) imekutana
katika Kikao cha Pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) kwa lengo la kuimarisha usimamizi na maendeleo ya Vyama vya
Ushirika nchini.

Kikao hicho kimefanyika Julai 15, 2020 Jijijini
Dodoma katika makao makuu ya Tume ya Maendeleo Ushirika Tanzania,
ambapo ujumbe wa TAKUKURU uliongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Brigedia
Jenerali John Mbungo, na ujumbe wa TCDC uliongozwa na Mrajis wa Vyama
vya Ushirika na Mtedaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Dkt.
Benson Ndiege.

Kikao hicho kililenga kuainisha majukumu ya Tume
ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) na majukumu ya TAKUKURU ili
kuwa na uelewa wa pamoja katika kuimarisha usimamizi na maendeleo ya
Vyama vya Ushirika nchini.

TAKUKURU iliwasilisha Taarifa ya
Uchunguzi na Fedha zilizokusanywa na Taasisi hiyo kwa niaba ya Vyama vya
Ushirika nchi nzima baada ya kukabidhiwa kazi hiyo na Waziri wa Kilimo,
Mhe. Japhet Hasunga.

Wajumbe wa Kikao hicho vilevile walijadili
mfumo na utaratibu unaotumiwa na TAKUKURU katika urejeshaji wa fedha
zilizokusanywa kwenye Vyama vya Ushirika na kuangalia njia na mbinu za
kuzuia mianya ya wizi na ubadhirifu katika Vyama vya Ushirika. Aidha,
TAKUKURU na TCDC walikubaliana kuhusu maeneo ya kushirikiana kati ya
taasisi hizo mbili.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia
Jenerali John Mbungo, amepongeza ushirikiano uliotolewa na Tume ya
Maendeleo Ushirika kwa TAKUKURU wakati wakitekeleza maagizo ya viongozi
Serikali katika urejeshaji wa fedha kwenye Vyama vya Ushirika zilizokuwa
zimechukuliwa bila kufuata utaratibu.

“Tuleteeni matatizo na
changamoto zinazohusu ubadhirifu unaofanywa na baadhi ya watu
wanaoviibia Vyama vya Ushirika ili tushughulike nao na kuhakisha kuwa
mali za wanaushirika zinakuwa salama,” amesema Brigedia Jenerali Mbungo.

Mrajis
wa Vyama vya Ushirika, Dkt. Benson Ndiege amesema kuwa kazi iliyofanywa
na TAKUKURU katika katika urejeshaji wa fedha kwenye Vyama vya Ushirika
zilizokuwa zimechukuliwa bila kufuata utaratibu imewezesha kutoa ujumbe
mahsusi kuwa fedha na mali za Wanaushirika hazitakiwi kuchezewa.

“Tutaendelea
kushirikiana na TAKUKURU katika kuhakikisha kuwa mali za wanachama wa
Vyama vya Ushirika zinalindwa na kuwanufaisha Wananchi na Warajis
Wasaidizi wa Vyama vya Ushirika wa Mikoa na Maafisa Ushirika wa Wilaya
waendelee kushirikiana na Maafisa wa TAKUKURU katika maeneo yao ili
kulinda mali za Wanaushirika,” amesema Dkt. Ndiege.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )