TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA YAVISHAURI VYOMBO VYA HABARI

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora  imevishauri vyombo vya habari hususani runinga  kuweka kipengele cha msomaji wa habari wa lugha ya alama wakati wa kurusha matangazo yao ili watu  walemavu wa kusikia  (Viziwi) nao waweze kuelewa taarifa zinazotolewa kuhusiana na ugonjwa  na Ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona.

Akizungumza na Wanahabari  jijini Dodoma ,Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu  amesema  hali hiyo itatoa fursa kwa watazamaji wote wakiwemo wenye ulemavu kujua kinachoendelea huku pia akiipongeza wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na watoto na watendaji wake kwa kutoa huduma stahiki kwa wanachi ambao tayari wemekwisha  ambukizwa ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19).

Amesema jamii inapaswa kutokufanya mzaha na jambo hilo kwani janga hilo ni kubwa hivyo ni muhimu kuunga mkono jitihada za serikali kwa kufuata maelekezo sahihi  ikwemo wale wote washukiwa wa maambukizi na wenye maambukizi kukaa karantini kwa muda ulipangwa ili kuzuia

maambukizi ya ndani kuongezeka.

Tume hiyo pia imeendelea kuwaomba wadau mbalimbali kuendela kujitokeza kuunga mkono jitihada za serikali katika mapambano dhidi ya maradhi hayo huku akitoa ushauri kwa serikali kuendelea kuchukua tahadhari
katika mipaka ili kuzuia kuingia kwa maambukizi  mapya kutoka nje ya
nchi.

 Tume  hiyo pia imeipongeza Jumuiya ya asasi za kiraia  AZAKI na wafanyabishara waliojitokeza kuunga mkono jitihada za serikali katika kupambana na ugonjwa huo.

Hatahivyo, Tume hiyo imeendelea kuipongeza serikali  kwa juhudi kubwa inazofanya  ya kupambana na  mlipuko wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) .

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )