TULIA ACKSON AWAUNGA MKONO ITEZI UNITED

Mbunge wa Mbeya Mjini Dr. Tulia Ackson ameichangia team ya Itezi United inayoshiriki ligi ya mabingwa wa mikoa Tanzania Tsh: 500,000/- kwa ajili ya kuwawezesha kwenda katika mashindano hayo yanayaotarajiwa kuanza kufanyika katika Mkoa wa Lindi ambapo Itezi United inaenda kuwakililisha Mkoa wa Mbeya.

Wakati huohuo Dr. Tulia ametoa mchango wa bandu nne za bati katika ofisi ya CCM tawi la Mwasote iliyopo kata ya Itezi Jijini Mbeya ambayo ujenzi wake unaendelea kwa lengo la kuboresha miundombinu.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )