TFF “Hakuna mchezo wowote wa kirafiki utakaoruhusiwa”

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limesimamisha michezo yote ya kirafiki nchini mpaka pale itakapokutana na vilabu kwanza.

“Kuanzia sasa hakuna mchezo wowote wa kirafiki utakaoruhusiwa kuchezwa Tanzania bila ruhusa ya TFF.”

Leo June 09, 2020, TFF itakutana na vilabu vya Simba, Yanga, Azam, KMC na Trans Camp kujadili namna ya kujikinga na ugonjwa wa Corona kwa mwongozo uliotolewa na Wizara ya Afya.

Inadaiwa kuwa vilabu hivyo vimecheza mechi za kirafiki bila kufuata mwongozo wa Wizara ya Afya.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )