TETESI ZA USAJILI LEO JUMATANO, JUNE 10, 2020

~Mtendaji Mkuu wa klabu ya RB Leipzig, Oliver Mintzlaff amemuambia beki wa klabu hiyo, Dayot Upamecano asaini mkataba mpya au aondoke mwishoni mwa msimu huu.

Upamecano mkataba wake unafikia tamati mwaka 2021 na Leipzig hawataki kumruhusu beki huyo kuingia katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake bila mkataba mpya kwasababu watahatarisha kumpoteza bure.

Upamecano ana thamani ya Euro Milioni 60 kwenye mkataba wake ambayo inafikia kikomo Juni 30 mwaka huu.

~Manchester City wamejiunga katika mbio za kuwania saini ya beki wa kushoto wa Leicester City Ben Chilwell 23 ambaye anawindwa sana na Chelsea.

~Mkurugenzi wa Michezo wa PSG, Leonardo amemuambia nahodha wa klabu hiyo, Thiago Silva kwamba hatopawa mkataba mpya baada ya mkataba wake wa sasa utakapofika tamati mwishoni mwa msimu huu.

Silva alijiunga na PSG mwaka 2012 na baada ya miaka 8 kuchezea Paris sasa atakuwa mchezaji huru na kuondoka jijini Paris akiwa na umri wa miaka 35 .

~Mario Baloteli amezuiwa kuingia katika eneo la Uwanja wa mazoezi wa klabu ya Brescia ya Italia.

Siku ya Jumapili klabu hiyo ilitangaza kuvunja mkataba wa nyota huyo akidaiwa kutoroka mazoezi bila Taarifa.

~Klabu ya Chelsea inataka kumsajili kiungo mshambuliaji wa Bayern Leverkusen, Hai Havertz majira haya ya joto.

Leverkusen hawajapokea ofa rasmi kwa ajili ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 lakini inaaminika Real Madrid na Bayern Munchen wameshafanya mazungumzo na klabu hiyo.

Mpaka sasa Havertz ameshafunga magoli 11 na Assist 5 katika mechi 26 za Ligi Kuu ya Ujerumani msimu huu huku mkataba wake na Leverkusen ukifikia tamati 30 Juni, 2022.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )