Tanzia : MWANDISHI WA HABARI ELIYA MBONEA AFARIKI DUNIA

Mwandishi wa Habari wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd inayochapisha Magazeti ya Mtanzania,Rai, Bingwa na Dimba pamoja na Mtanzania Digital bwana Eliya Mbonea amefariki dunia leo Jumatatu Aprili 6,2020 wakati akiendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari mkoa wa Arusha (Arusha Press Club), Claude Gwandu amethibitisha taarifa za kifo cha Eliya Mbonea alipozungumza na Malunde 1 blog mchana huu.

“Ni kweli ndugu yetu Elia Mbonea ametutoka mchana huu. Alikuwa anaendelea na matibabu katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kumtoa hospitali ya KCMC hivi karibuni. Tutapeana taarifa zaidi baadaye”,amesema Gwandu.

Mungu Ailaze Mahali Pema Peponi Roho ya Marehemu Elia Mbonea. Amina
CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )