TANZIA: Mchungaji wa Kanisa la Mlima wa Moto Getrude Rwakatare Afariki Dunia

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) na Mchungaji wa Kanisa la Mlima wa Moto (Mikocheni B Assemblies of God ) Mchungaji Dkt.Getrude Rwakatare amefariki dunia Alfajiri ya leo.


Kwa mujibu wa mtoto wake Muta Rwakatare amesema marehemu alikuwa akisumbuliwa na Presha.

“Ni bahati mbaya imetokea asubuhi ya leo saa 11 kasoro, alikuwa na matatizo ya moyo, jana tulimkimbiza Hospitali lakini bahati mbaya imetokea, tupo katika hatua ya kuangalia namna gani tutafanya ili tuweze kumpumzisha mama yetu” amesema Muta.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )