TAMASHA LA KUIBUA VIPAJI SHULENI LAFANYIKA BRAEBURN INTERNATIONAL SCHOOL ARUSHA

 

Na Ferdinand Shayo ,Arusha.

Tamasha kubwa  la kuibua vipaji shuleni limefanyika katika shule ya Braeburn international School Arusha likihusisha michezo mbali mbali ikiwemo sarakasi,maigizo pamoja na kucheza muziki huku likihudhuriwa na mamia ya wazazi wa wanafunzi wanaosoma shuleni hapo.

Wanafunzi walioshiriki mchezo wa sarakasi maarufu kama (trapeze) akiwamo Cherim Lim amesema kuwa kushiriki tamasha hilo kumemsaidia kukuza kipaji chake cha sarakasi na kuionyesha jamii kuwa inawezekana kufanya vitu vikubwa duniani.

 “Nimefanya mazoezi kwa kipindi cha miezi minne sasa michezo hii inasaidia kuongeza ujasiri na nidhamu ,Zaidi tamasha hili linatoa fursa kwa wanafunzi kuonyesha vipaji vyao”Anaeleza Cherim

Mshiriki wa Maigizo Lee Filikunjombe amesema vipaji walivyonavyo vinaweza kuwasaidia kutumia vipaji vyao kama fursa ya ajira kwani michezo ni burudani na ni ajira pia.

Mwalimu wa Sanaa katika Shule ya Braeburn International School Arusha Miranda Rashid amesema kuwa wanafunzi wa shule hiyo wana vipaji kweli ,wamekua wakifanya kazi ya kuvumbua vipaji hivyo na kuviendeleza ili viweze kukua.

“Kwa sasa tuna shule maalumu ya Sanaa ambayo kazi yake ni kukuza na kuendeleza vipaji vya wanafunzi wetu” Anaeleza Miranda.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )