TALIRI YAJIKITA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFUGAJI NCHINI

 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dkt. Jonas Kizima (katikati- aliyevaa suti nyeusi) akijadiliana jambo na baadhi ya Viongozi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Maafisa wengine wa kituo cha TALIRI Mpwapwa alipotembelea kituo hicho jana.

Kaimu
Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dkt.
Jonas Kizima (katikati- aliyevaa suti nyeusi) akijadiliana jambo na baadhi
ya Viongozi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Maafisa wengine wa kituo
cha TALIRI Mpwapwa alipotembelea kituo hicho jana.

Baadhi
ya Ng’ombe wanaofugwa katika kituo cha TALIRI Mpwapwa kilichopo Wilayani
Mpwapwa wakinywa maji katika kisima kilichotengwa kando ya Josho la Nunge
kwa ajili ya kunyweshea mifugo.
Mkurugenzi
wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Huduma za Ugani, Dkt. Angello Mwilawa akiwaeleza
Waandishi wa Habari (hawapo pichani)  
kuhusu utafiti wa malisho unaofanywa na
Kituo cha Utafiti wa Mifugo (TALIRI) Mpwapwa kilichopo Wilayani Mpwapwa
alipotembelea
   moja ya Shamba la
Malisho ya mifugo la kituo hicho jana. Kulia kwake ni Kaimu
Mkurugenzi Msaidizi, Utafiti na Mafunzo, Dkt. Hassan Mruttu.

 


Na Mbaraka Kambona, Mpwapwa

 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Taasisi
ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dkt. Jonas Kizima amesema utafiti wanaoufanya
umejikita katika kutatua changamoto za mbegu bora za mifugo na mbegu bora za
malisho kwa wafugaji ili sekta ya mifugo iweze kuchangia vyema katika pato la
Taifa.
 

Dkt. Kizima aliyasema hayo alipotembelea kukagua
shughuli zinazofanywa na Kituo cha TALIRI Mpwapwa kilichopo Wilayani Mpwapwa,
Mkoani Dodoma jana.
 

Alisema kuwa lengo la
utafiti wanaoufanya ni kuhakikisha wanapata mbegu bora za mifugo na kuzalisha
mbego bora za malisho ya mifugo ambazo zitakazosaidia kutatua changamoto za
upatikanaji wa mbegu bora za mifugo zinazohimili mazingira yaliyopo na malisho
inayoikabili nchi kwa sasa.
 

Aliongeza kuwa kwa sasa
taasisi hiyo inaendelea na kufanya Tathmini ya ubora, ustahimilivu na makuzi ya
malisho ya mifugo yatakayofaa kwa chakula cha kutosha kwa ajili ya mifugo.
 

Kwa mujibu wa Dkt. Kizima, matokeo
yoyote ya utafiti lazima yabadilishwe kuwa biashara kwa sababu wafugaji wakifanya
ufugaji unaoendana na mazingira yao itawasaidia kutengeneza uchumi na kuwaongezea
tija katika ufugaji wao.
 

“Tafiti tunazozifanya
zinalenga kuimarisha mnyororo wa thamani wa mifugo ili mchango wa sekta ya
mifugo uweze kuonekana katika uchumi wa kati,” alisema Dkt. Kizima.
 

Dkt. Kizima alisema kuwa TALIRI
imesambaza vituo vyake katika Kanda Saba nchini ili kuwa karibu na wafugaji
kuwasaidia kutatua changamoto zao ili waweze kufanya ufugaji wenye tija.
 

Alisema vituo hivyo vipo
katika Kanda ya Mashariki, Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Kati, Kanda ya Kusini,
Kanda ya Magharibi, Kanda ya Ziwa na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.
 

Naye, Mkurugenzi, Idara ya Utafiti,
Mafunzo na Huduma za Ugani, Dkt. Angello Mwilawa alisema kuwa Wizara ya Mifugo
na Uvuvi imezihamasisha Halmashauri zote nchini kuanzisha mashamba darasa ya
malisho ili wafugaji waweze kujifunza na kupata mbegu bora za malisho kwa ajili
ya mifugo.
 

“Tunawahimiza wafugaji
kuona umuhimu wa kulima malisho ili yaweze kuwasaidia kupata lishe ya uhakika
kwa mifugo yao na pia kwa kulima malisho kutawapunguzia migogoro ya mara kwa
mara kati yao na wakulima,” alisema Dkt. Mwilawa.
 

Aliongeza kuwa wanawahamasisha
wafugaji hususan walio katika nyanda kame wastawishe malisho ya mifugo wakati
wa masika na kuyatunza ili yaweze kuwasaidia kulisha mifugo yao wakati wa
kiangazi.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )