TAKUKURU wilaya ya Kiteto yasaidia kurejesha Mahindi ya Kijiji.

Na John Walter-Manyara
Taasisi ya kuzuia na
kupambana na Rushwa  wilaya ya Kiteto
mkoa wa Manyara ,imefanikiwa
kurejesha  mahindi gunia 45 katika kijiji
cha Loltepes.

Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya
Kiteto Venance Sangawe amesema mahindi  hayo ni sehemu ya gunia 90 ambazo
Takukuru  iliingilia kati kurejesha.

Sangawe amesema  diwani wa kata ya Sunya  aliemaliza muda wake, Musa Brayton na
mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi  katika
 kata hiyo Abdi Puputo  walishindwa kutimiza masharti waliyokubaliana
na kijiji  ya  kulipa mahindi hayo baada ya kulima shamba la
kijiji  ekari tisini.

Ameongeza kuwa makubaliano
kati ya watu hao na kijiji ilikuwa ni kulipa gunia moja kwa kila ekari tangu mwaka 2017  hivyo kwa kushindwa kufanya hivyo Takukuru
imeamua kuisaidia kijiji kurejesha mahindi hayo.

Akikabidhi mahindi hayo kwa
mwenyekiti wa kijiji cha Loltepes Mkuu wa wilaya ya Kiteto Tumaini Magessa,  amewataka viongozi wa kijiji na shule kuhakikisha
mahindi hayo yanatumika kwa ajili ya chakula cha wanafunzi wa shule za Loltepes
na Loiborsoit zilizopo katika kijiji hicho.

Huo ni mwendelezo wa
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Manyara katika kurejesha na
kukabidhi mali kwa wahusika halali ili  kuondoa  migogoro isiyokuwa ya lazima.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )