TAKUKURU kuwafikisha Mahakamani Vigogo wa NEMC

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU), inawafikisha watumishi wanne wa Baraza la Taifa la Uhifadhi wa
Mazingira (NEMC) katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa
tuhuma za rushwa na uhujumu uchumi.Watuhumiwa hao ni; Deusdedith
Katwale, Magori Matiku na Obadia Machupa ambao wote ni maafisa mazingira na
Lydia Nyinondi ambaye ni Mhasibu Msaidizi. Wote wa makao makuu.

Taarifa iliyotolewa leo Juni 4 mwaka 2020 na
Afisa Uhusiano wa Takukuru, Doreen Kapwani imesema, kuwa watuhumiwa hao,
watasomewa mashtaka yao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es
Salaam.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )