Taasisi yakabidhi vifaa vya kujikinga na Corona Jeshi la Magereza Mbeya

Na Esther Macha ,Mbeya

TAASISI ya Tulia Trust imetoa msaada wa vifaa kwa ajili ya kujikinga  na COVID 19 kwa Jeshi la magereza Jijini Mbeya ili kuweza kusaidia mikusanyiko ya watu katika maeneo hayo.

Akipokea vifaa hivyo katika Gereza la Ruanda Jijini Mbeya kwa niaba ya Jeshi la Magereza Mkoani hapa, Mathias Mkama aliishukuru Taasisi ya Tulia Trust kutoa vifaa hivyo ambavyo ni ndoo,vitakasa mikono na vizibao(reflector) kwa ajili ya mafundi.

Alisema vifaa hivyo vimekuja kwa wakati na alisema kutoa ni moyo usambe ni utajiri hivyo wadau wengine waige mfano wa Taasisi ya Tulia Trust.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Meneja wa Tulia Trust ,Jacqueline Boaz alisema Magereza ni Taasisi kubwa inayokabiliwa na mkusanyiko wa watu wengi hivyo kama Taasisi iliona umuhimu wa kutoa msaada huo.

Boaz alisema vifaa vilivyotolewa ni pamoja na sabuni chupa arobaini,ndoo ishirini na vizibao(reflector) ishirini.

Hata hivyo alisema Taasisi yake itaendelea kutoa msaada kwa magereza kadiri inavyopata fursa.

Sabuni zilizotolewa katika Gereza zilitolewa kwa ufadhili wa Star Tika ambayo ni moja ya kampuni zinazoshirikiana na Taasisi ya Tulia Trust.

Hivi karibuni Taasisi ya Tulia Trust ilitoa mabati kwa ajili ya ujenzi wa banda la kupumzikia wageni ambapo banda la awali lilikuwa ni dogo na chakavu na sasa banda hilo linatumika.

Mwisho.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )