SHULE YA SEKONDARI YA MFANO NCHINI YAANZA RASMI.

Wanafunzi 136 wenye Mahitaji Maalumu kunufaika na elimu ya Sekondari baada ya kuanza  rasmi kwa  shule ya Sekondari  ya mfano nchini ya Patandi Maalumu iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya  Meru  Wilayani Arumeru, Mkoani Arusha.

  

Ndugu Emmanuel Mkongo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru , ameishukuru Serikali kwa kwa kujenga miundombinu ya madarasa ,mabweni,ofisi ya walimu ,maabara, na 

maktaba  kwani ni sehemu ya  mafanikio makubwa  katika  kuhakikisha kila mtoto wa Tanzania anapata elimu wakiwemo watoto wenye Mahitaji Maalum yanatimia.

Mkongo amepongeza juhudi za timu kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI , Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia pamoja Wataalam wa Chuo Cha Ualimu Patandi na Wataalam wa Halmashauri katika kuhakikisha miundo mbinu muhimu na rafiki kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum inakamilika.

Mkongo ametoa wito kwa Wazazi wa wanafunzi waliopangwa shule hiyo kuhakikisha wanaripoti kwa wakati na ili wanafunzi waweze kuanza masomo.

Shule  ya  Sekondari Patandi Maalumu  imepangiwa wanafunzi 185 wakiwemo wanafunzi wa Kutwa 49 na  wanafunzi  wa bweni  wenye mahitaji maalum 136.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )