SHILATU ARIDHISHWA NA UANDIKISHWAJI WAPIGA KURA

 Na Mwandishi wetu Mihambwe


Zoezi la uandikishwaji na uboreshwaji wa Wapiga kura kwenye daftari la kudumu la Wapiga kura limeenda vyema kwa amani na utulivu.


Hayo yamejidhihirisha kwenye ziara aliyoifanya Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu alipotembelea na kukagua vituo mbalimbali vya uandikishaji ambapo alijionea amani na utulivu ikitawala huku Watu wengi wenye sifa wakijitokeza kuandikisha na wengine kufanya maboresho ya taarifa zao.

“Huu ni mzunguko wa awamu ya pili ya uandikishaji ambapo amani imetawala, Wananchi wakijitokeza kwa wingi kujiandikisha na wengine kuboresha taarifa zao kwenye daftari la kudumu ili wapate sifa ya kuwachagua viongozi wanaowataka kwenye uchaguzi mkuu. Makundi rika ya jinsia zote wamejitokeza.” Alisema Gavana Shilatu.

Katika ziara hiyo Gavana Shilatu aliambatana na baadhi ya Wajumbe kamati ya ulinzi na usalama ya Tarafa ambapo Wananchi wengi wamepongeza zoezi lilivyoendeshwa na kusimamiwa vyema ndani ya Tarafa ya Mihambwe.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )