SHILATU AKAGUA UJENZI NYUMBA YA MWALIMU, WANANCHI WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI

Na Mwandishi wetu Mihambwe

Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu amekagua ujenzi nyumba ya Mwalimu huku Wakazi wa Kijiji cha Mpunda kilichopo kata ya Michenjele wakimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwajengea nyumba ya kuishi Mwalimu katika shule ya msingi Mpunda.

“Tunamshuru Rais Magufuli kutuletea fedha za kujenga nyumba hii ya Mwalimu. Haijawahi kutokea tangu tupate Uhuru maendeleo haya ya kasi tunayoyaona. Pia tunamshukuru Afisa Tarafa Mihambwe kututembelea mara kwa mara kujua maendeleo ya mradi huu.” alisema Mzee Issa Mohammed Mnindanga (65)

Naye Mwalimu wa shule hiyo alimshukuru Rais Magufuli kuwapunguzia kero ya makazi ya kuishi mbali.

“Namshukuru sana Rais wetu John Pombe  Magufuli kutupunguzia kero ya makazi sisi Waalimu. Tunampenda na tunamwahidi ushirikiano nae.” Alisema Mwalimu Flower Valentine Kibombo wa shule ya msingi Mpunda.

Gavana Shilatu  aliwasisitiza kamati kuwa Makini na mradi huu wa ujenzi na mafundi kujenga kwa kasi na viwango vinavyoendana na thamani ya fedha.

“Nami naungana na Wananchi hawa kumshukuru Rais Magufuli kutuletea fedha Tsh milioni ishirini na tano (25,000,000/=) za kujenga nyumba ya Kwanza kabisa ya Mwalimu kijijini hapa tangu tupate Uhuru. Kuhusu ujenzi sipendi kusikia fundi unachakachua mradi na kamati ihakikishe inapokea vifaa vyote toka kwa Mzabuni kama ambavyo vimeainishwa kwenye BOQ. Muwe wakali na huu mradi ukamilike.” Alisisitiza Gavana Shilatu wakati akiongea na Kamati ya ujenzi na uongozi wa shule.

“Kama fundi ninahaidi kujenga kwa uaminifu na kwa ubora na vifaa nitakavyokabidhiwa nitavitumia vyote pasipo kuvichakachua.” Alisema Fundi msimamizi Hamza Kaume.

Gavana Shilatu alifanya ziara ya kikazi kukagua mradi huo wa ujenzi wa nyumba ya Mwalimu ulioanza kwa nguvu ya Wananchi Tsh. Milioni nane na Rais Magufuli kutoa fedha Tsh. Milioni ishirini na tano za kumalizia mradi huo na kufanya gharama kuu za mradi huo kuwa Tsh. Milioni thelathini na tatu. Mradi huo unatarajia kukabidhiwa rasmi  mwezi Juni, 2020 tayari kwa matumizi.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )