SERIKALI YATANGAZA BEI ELEKEZI YA CHANJO 13 ZA MAGONJWA YA MIFUGO,WAZIRI MPINA AIPA KIBARUA KIZITO BODI YA TVLA

 Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akimkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti
mpya wa Bodi ya Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA), Profesa
Amandus Muhairwa baada ya kuiziduia bodi hiyo na kupokea taarifa ya
kutangazwa kwa bei elekezi ya Chanjo Makao Makuu ya Wizara ya Mifugo na
Uvuvi Mtumba jijini Dodoma

 Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akimkabidhi vitendea kazi Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) baada ya
uzinduzi wa Bodi ya TVLA Makao Makuu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi,
Mtumba jijini Dodoma.

Wajumbe
wa Bodi ya Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) wakiwa
katika picha ya pamoja na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ullega mara baada ya uzinduzi wa
bodi hiyo Makao Makuu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mtumba jijini Dodoma

Na
Mwandishi Wetu, Dodoma

SERIKALI
imetangaza bei elekezi ya chanjo 13 za magonjwa ya mifugo ya kimkakati ambapo sasa
wafugaji watapa ahueni kubwa kwa kutumia gharama ndogo kupata chanjo hizo  huku Waziri wa Mifugo na
Uvuvi, Luhaga Mpina akitaka bodi ya Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania
TVLA kuhakikisha Kliniki za mifugo zinajengwa kwenye halmashauri 185 kote nchini
ifikapo Juni 2021.

Akitangaza
bei elekezi wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakala wa Maabara ya Veterinari
Tanzania (TVLA) Dodoma, Mkurugenzi
wa Huduma za Mifugo  Tanzania, Profesa
Hezron Nonga amesema bei hiyo itaanza kutumika leo na kwamba wafugaji na
wafanyabiashara wote wanapaswa kufuata bei hiyo iliyotangazwa na Serikali.

Prof.
Nonga amezitaja  bei elekezi hizo kuwa ni
pamoja ya Chanjo ya Homa ya Mapafu ya Ngombe (CBPP) bei ya dukani kwa dozi
itauzwa sh. 300 huku bei ya uchanjaji kwa mfugo ikiwa ni sh. 550, Chambavu
(Black quarter) dozi dukani shilingi 500 kwa mfugo atachanjiwa sh. 800

Profesa Nonga amesema Kimeta (Anthrax) dozi dukani ni 250
na kwa mfugo itakuwa sh. 500, Mchanganyiko wa Chambavu na Kimeta (TECOBLAX)
 kwa Ng’ombe dozi dukani sh. 560 na kwa mfugo utachanjwa kwa sh.  800, Mchanganyiko wa Chambavu na Kimeta
(TECOBLAX)  kwa mbuzi na kondoo dozi kukani sh. 280 kwa mfugo ni sh. 500.

Pia ugonjwa wa Kutupa Mimba (Brucellosis) dozi dukani ni
1,000 na kwa mfugo ni 1,500,  Mdondo
(Newcastle disease) dozi ni shilingi 50 na mfugo ni 50, Mapele Ngozi (Lumpy
Skin Disease) kwa ng’ombe dozi dukani ni sh. 400 na kwa mfugo ni sh. 600 huku Sotoka
ya Mbuzi na Kondoo (PPR) dozi dukani ni sh. 200 na kwa mfugo ni 350.

Pia Homa ya mapafu ya mbuzi (CCPP) dozi dukani ni 200 na
mfugo itakuwa ni  350, Ugonjwa wa Miguu
na Midomo (FMD) dozi dukani ni sh. 2,500 na kwa mfugo ni 3,000, Kichaa cha Mbwa
(Rabies) dozi dukani ni 1,000 kwa mfugaji ni sh. 1,500.

Profesa Nonga ameongeza kuwa ugonjwa wa Ndigana Kali
(ECF) dozi dukani ni sh. 10,000 na kwa mfugo ni sh. 17,000
huku Homa ya Bonde la Ufa (RVF) dozi dukani ni sh. 400 huku kwa mfugo ikiwa ni
sh. 700.

Akizungumza
mara baada ya kuzindua Bodi hiyo ya TVLA, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga
Mpina amesema kupitia mabadiliko hayo ya Kanuni za kutoa bei elekezi, Serikali
itakuwa imepunguza gharama kwa wafugaji kutoka shilingi bilioni 482.4 walizokuwa
wakizutumia kununua chanjo hadi kufikia shilingi bilioni 237 ikiwa ni punguzo
la asilimia 51.

Hivyo
ameitaka bodi hiyo mpya kufanya kazi usiku na mchana  kuwalea wafugaji wa
Tanzania kupitia eneo hilo muhimu la chanjo na matibabu ya mifugo na
kukuchochea ungezeko la uzalishaji mifugo hali itasaidia kuhudumia viwanda vya mazao
ya mifugo vinavyojenga maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya kupeleka kwenye
masoko mbalimbali duniani.

Pia
ameitaka bodi hiyo kukomesha matumizi ya dawa feki na zilizomaliza muda wake ,
kurahisisha upatikanaji wa chanjo hatua itakayowezesha kuendelea kupungua kwa
magonjwa na kuweza kuongeza masoko na ushindani kimataifa.

Mpina
ameigiza bodi hiyo kuhakikisha kuwa ifikapo Juni, 2021 chanjo 7 ambazo ziko
katika hatua mbalimbali zizalishwe hapa nchini ili kuwawezesha wafugaji
kuzipata kwa urahisi na kwa gharama nafuu.

Pia
Waziri Mpina ameitaka bodi huhakikisha kuwa ujenzi wa Kliniki za mifugo kwa
halmashauri zote 185 kote nchini pamoja na mikoa 15 ambayo haina maabara kwa
sasa ziwe zimekamilika ifikapo Juni 2021.

Mwenyekiti
wa Bodi ya TVLA, Profesa Amandus Muhairwa amemhakikisha Waziri Mpina kuwa
watatumia weledi wao wote kuhakikisha wanatekeleza maagizo yote aliyoyatoa ili
kuiwezesha Sekta ya Mifugo kupita hatua kubwa kwa kipindi chote cha uongozi
wao.

Wajumbe
wengine wa  Bodi hiyo ni  Dk. Haruni Mapesa kutoka Chuo Kikuu Mzumbe,
Dk. Akida Khea kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Casmir Kyuki kutoka
Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania na Selina Lyimo ambaye ni Mkurugenzi wa
Utawala na Rasilimali Watu(Mstaafu).
CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )