SERIKALI KUJENGA KITUO KIKUBWA CHA UKUZAJI VIUMBE MAJI CHATO

Mkuu
wa Wilaya ya Chato Mhe. Charles Kabeho akizungumza na ujumbe kutoka
Wizara ya Mifugo na Uvuvi na taasisi ya ujenzi ya Corporation sol
uliofika ofisini kwake muda mfupi kabla ya kuelekea kijiji cha
Rubambangwe ambako kitajengwa kituo kikubwa cha kukuzia viumbe Maji.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dokta Rashid Tamatamah (Kulia)
akionesha mipaka ya eneo kinapotarajiwa kujengwa kituo cha kukuzia
viumbe hai katika kijiji cha Rubambangwe wilayani Chato muda mfupi kabla
ya kukabidhi eneo hilo kwa mkandarasi (Corporation Sol) ili aweze
kuanza ujenzi wa kituo hicho.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dokta Rashid Tamatamah (kulia)
akikabidhi mkataba na michoro ya majengo ya kituo cha kukuzia viumbe
maji kwa Meneja wa Kampuni ya Corporation Sol Bw. Simeo Machibya
Wilayani Chato (Geita).

Wizara
ya Mifugo na Uvuvi kupitia sekta ya Uvuvi imeikabidhi kampuni ya
ukandarasi ya Serikali ya Corporation Sol eneo naf mkataba wa Ujenzi wa
Kituo kikubwa cha Ukuzaji wa Viumbe Maji ili kazi hiyo ianze mara moja.

Makabidhiano
hayo yaliyofanyika leo (08.07.2020) katika kijiji cha Rubambangwe
kilichopo Wilaya ya Chato mkoani Geita yalifanywa na Katibu Mkuu Wizara
ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dokta Rashid Tamatamah ambaye mbali na
kubainisha kuwa mradi huo utakuwa ni mkubwa kuliko yote hapa nchini, pia
alielezea maeneo kadhaa yatakayohusiana na mradi huo.

Dokta
Tamatamah alisema kuwa mradi huo utajumuisha ujenzi wa mabwawa
yatakayokuwa na uwezo wa kutoa zaidi ya tani 10 kwa mwaka, jengo la
vitotoleshi vya samaki ambalo litakuwa na uwezo wa kutoa vifaranga zaidi
ya milioni mbili kwa mwaka, jengo dogo la kutengeneza chakula cha
samaki na eneo la kuhifadhia samaki hao.

Aliongezea kuwa mradi
huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 3.8 mpaka kukamilika kwake na
tayari Wizara ilishalipa fidia ya shilingi milioni 42 kwa wakazi
waliokuwa wakifanya shughuli zao za kiuchumi katika maeneo hayo yenye
ukubwa wa zaidi ya ekari 28.

“Lakini pia hapa litajengwa darasa,
bweni na ukumbi wa chakula kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wakuzaji
viumbe maji wanaohitaji kujifunza au kuongeza ujuzi wa taaluma hiyo kwa
kozi fupi za wiki mbili au tatu” Alisistiza Dokta Tamatamah.

Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Ukuzaji Viumbe Maji ambao ndio wasimamizi
wakuu wa kituo hicho pindi kitakapoanza kufanya kazi, Bw. Nazaeli Madala
alisema kuwa kituof hicho kitakuwa ni ufumbuzi wa changamoto ya uchache
wa samaki wanaopatikana kwenye vyanzo vya asili.

“Kituo hiki
kitahudumia mikoa yote inayozunguka kanda ya ziwa na maeneo jirani na
ukanda huo na tutawafundisha wafugaji wa samaki, maafisa ugani wa fani
ya ufugaji wa samaki na pia kitatumika kwa ajili ya mafunzo ya vitendo
kwa wanafunzi wanaosoma katika ngazi mbalimbali huko vyuoni” Aliongeza
Madala.

Madala alibainisha kuwa kituo hicho kitawasaidia kupata
muongozo wa kujenga vituo vingine katika maeneo yanayozunguka Ziwa
Tanganyika, Nyasa na maeneo ya Pwani lengo likiwa ni kuhakikisha viwanda
vyote vya samaki vilivyopo nchini havikosi malighafi.

Naye Afisa
Mtendaji wa kijiji cha Rubambangwe Bi. Restituta Majura alisema kuwa
mradi huo utawanufaisha sana wakazi wa kijiji hicho kwani mbali na kutoa
ajira kwa wananchi watakaoshiriki kwenye hatua ya ujenzi, pia
wanatarajia kunufaika na uwepo wa barabara itakayoelekea eneo la mradi
kwani pia itawasaidia kufika kwenye zahanati ya kijiji inayoendelea
kujengwa hivi sasa.

Kabla ya kuelekea kwenye eneo la ujenzi wa
kituo hicho, Dokta Tamatamah akiwa na timu yake ya wataalam kutoka
Wizarani walifika ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Charles
Kabeho ambaye aliishukuru Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kupeleka mradi
huo kwenye Wilaya yake na kuahidi kufuatilia kwa ukaribu hatua zote za
ujenzi wa kituo hicho hadi kitakapokamilika mnamo mwezi Oktoba mwaka
huu.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )