RPC TANGA WAONYA WEZI,AWAAMBIA WAKAOKAMATWA WATAWAFINYANGAFINYANGA WASAHAU WALIPOTOKEA

KAMANDA
 wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP)
Blasius Chatanda akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali

 KAMANDA
 wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP)
Blasius Chatanda akiwaonyesha waandishi wa habari vitu ambavyo
vimekamatwa wakati wa opeseheni hiyo


Camera ambazo pia zimekatwa wakati wa operesheni hiyo

KAMANDA
 wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP)
Blasius Chatanda ametoa onyo kali kwa wezi wanaovunja nyumba za watu na
kuiba mali kwa kuwataka waache mara moja tabia hiyo kabla
hawajawafinyangwa finyangwa.

Chatanda aliyasema hayo wakati
akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kwamba awali kulikuwa
kumeibuka wimbi la uvunjaji wa nyumba hali ambayo iliwalazimu kuanzisha
operesheni kabambe ya kuwasaka ili kuhakikisha wananchi wanaishi kwa
amani.

Alisema kwamba katika operesheni hiyo walifanikiwa
kuwakamata watuhumiwa 8 ambao kwa sasa wapo mahabusu ambapo walikamatwa
wakiwa na vitu mbalimbali ambavyo waliviiba kwenye maeneo mbalimbali
Jijini Tanga.

Kamanda Chatanda alitaja vitu ambavyo vilikamatwa
kuwa ni TV Flat Screen 7zenye ukubwa wa tofauti kuanzia nch 50
 hadi 21 ambazo zinadaiwa ziliibiwa kwenye baadhi nyumba za kulala
wageni zilizopo Jijini Tanga.

Aidha alisema pia katika
operesheni hiyo waliwakamata vitu vingine ikiwemo Kompyuta mpakato
16,simu za mkononi 7 ambapo baadhi ya vitu hivyo viliibiwa kwenye nyumba
 za kulala wageni.

“Tunaomba walioibiwa waje watambue mali zao
kama ni miongoni mwa zilizokamatwa huku akisisitiza kwamba msako huo ni
endelevu na hakuna mtu ambaye hatabaki salama “Kamanda wa Polisi Mkoa wa
 Tanga.

Kamanda huyo alisema kwamba msako huo ni endelevu na
hakuna mtu ambaye atabaki salama huku akieleza kwamba kwa waliozoea
kuiba watafute kazi nyengine za kufanya kwa sababu wakikamatwa
watawafinyangwafinyanwga mpaka wasahau njia walizokujia.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )