RIDHIWANI KIKWETE AMPA HEKO WAZIRI WA MAJI JUMA AWESU, AMUOMBA KUMALIZA TATIZO LA MAJI CHALINZE

 

NA ANDREW CHALE, DODOMA.

MBUNGE Jimbo la Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete amempongeza Waziri wa Maji, Juma Awesu kwa kuitendea haki Wizara hiyo ambapo pia amemuomba kuongeza kasi katika kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji kwa kukamilisha miundombinu ya miradi ya maji inayojengwa katika Jimbo hilo la Chalinze.

Ridhiwani Kikwete amebainisha Bungeni wakati wa kujadili Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Ufunguzi Rasmi wa Bunge la Kumi na Mbili.

“Nitumie nafasi hii kumpongeza sana ndugu yangu Bwana Awesu Waziri wa maji kwa kazi nzuri sana anayoifanya. Wana Chalinze wanakushukuru na wanaendelea kushukuru kwa kiasi kikubwa unayoendelea kuyafanya.

Wito wao mmoja tu, ni kwamba zile pampu zinazojengwa pale Msoga na pale  Chamakweza wanaomba ziharakishwe  kuona zinakamilika mapema ili lile tatizo la maji linalowakabiri wananchi wale liweze kuisha na liwe hadithi ambayo imepita.” Alisema Ridhiwani Kikwete wakati wa kuunga mkono hoja pamoja na kuunga mkono Hotuba ya Rais.

Serikali kupitia Wizara yake hiyo ya Maji na Mamlaka ya Maji DAWASA,  tayari wapo katika ujenzi wa vituo vya kusukuma maji (buster stations)  na pamu kwenye maeneo ya Chamakweza na Msoga ambapo mradi huo utakapokamilika utamliza tatizo la maji Jimbo la Chalinze pamoja na maeneo ya jirani ikiwemo Morogoro Vijijini.

Mwisho.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )