RDO WAJA NA UBUNIFU WA MASK (BARAKOA) ISIYOCHOKA MAPEMA

Mafundi wa shirika la lisilo la  kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Mufindi na  Kilolo  mkoani  Iringa wakionesha mask (barakoa ) walizotengeneza kwa kutumia vitambaa ambazo ni bora zaidi na unaweza kuzifua

…………………………………….


KATIKA kukabiliana na changamoto ya uhaba wa Mask (barakoa)mitaani shirika la lisilo la  kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Mufindi na  Kilolo  mkoani  Iringa limeanzisha  utengenezaji wa barakoa hizo ili kusaidia jamii kujinginga na maambukizi ya  virusi vya Corona    mkoani hapo na nje ya  mkoa .
Akizungumza  jana waandishi wa habari     mkurugenzi wa shirika    RDO Fidelis Filipatali   alisema  kuwa   wamelazimika   kuanzisha  utengenezaji wa barakoa   baada ya  kuona   uhitaji  wa  barakoa  ni mkubwa na upatikanaji wake ni mgumu na hata kama  zinapatikana  gharama yake ni  kubwa  ambayo  wananchi  wenye uchumi wa chini na wale wasio na kipato wamekuwa  wakishindwa  kumudu gharama  ya  kununua barakoa   hizo .
Hivyo  alisema  wamefanikiwa  kubuni barakoa za  kisasa  za kujinginga na gonjwa  la Covid 19   ,barakoa ambazo unaweza  kuzitumia  kwa  muda  mrefu  zaidi bila  kuzitupa maana  hizo ambazo  wanazitengeneza  wamezitengeneza  kwa ubora  zaidi na mtumiaji anaweza  kuzifua mara kwa mara  na kuzitumia  tena pasipo tatizo  lolote .
Filipatali  alisema   shirika   hilo  limekuwa likizitengeneza barakoa  hizo kwa  kuwatumia  watoto  ambao  wanatoka katika mazingira  magumu  ambao  wamekuwa  wakifundishwa ufundi  mbali mbali kupitia  chuo chake kilichopo Mdabulo , Mafinga na Kilolo japo  kiwanda  cha  kutengeneza barakoa  hizo  kipo  mjini Mafinga .
” TUnachohitaji  kuwezeshwa  kupata vitambaa vya  kutosha  na vifaa zingine  kwa ajili ya kutengenezea barakoa  hizi na kama  tutawezeshwa  tunao uwezo wa  kuzalisha barakoa  kwa wingi na  kuzigawa bure ama  kwa kuziua kwa gharama ndogo  zaidi   kwenye  taasisi  mbali mbali na  wananchi wa vijijini na mijini  wenye kipato cha  chini  ili  waweze kuzitumia  kujikinga na  maambukizi ya virusi  hivi hatari vya Corona ” alisema 
Kwa  sasa  wameweza  kutengeneza barakoa kwa  ajili ya matumizi ya shirika   hilo  badala ya  kuhangaika  kununua madukani kwa  gharama  kubwa ya shilingi 15000 kwa  barakoa ya  bei ya  juu ambayo unaweza kutumia kwa siku  mbili  wao  wanatengeneza  wenyewe barako   za  kisasa  zaidi  za  kutumia hata  kwa miezi mitatu na kuendelea  pasipo  kupoteza ubora  wake .
Hata   hivyo  alisema kuwa RDO  kupitia  vyuo  vyake  vya  vya ufundi  stadi  wameendelea   jihusisha na kutoa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana hasa waliopo vijijini kwa lengo la kuwawezesha kupata ujuzi mbalimbali wa mafunzo ya Ufundi Stadi ili waweze kuendana na sera ya uchumi wa viwanda kwa kuongeza idadi ya watu kujitegemea wao wenyewe, familia zao, jamii inayowazunguka na taifa kwa ujumla kwa kujiajiri wao wenyewe na kuajiriwa nakwa   kupitia gonjwa  hilo la Covid 19 wameendelea  kubuni mbinu ya kujikinga na kuwakinga  wananchi na virusi vya Corona .
Alisema  ubunifu mbali mbali  wanaoufanya  unapelekea  vijana zaidi ya 300   kupenda  kuishi mazingira ya vijijini na kuto kimbilia  mijini na nchi za nje badala  yake  wanaweza kujiajiri  wenyewe  huko huko  vijijini kupitia fani mbali mbali  walizopewa  .
  
Hata   hivyo  pamoja na kubuni kutengeza barakoa alisema   chuo   kabla ya  kufungwa  kwake  kwa agizo la serikali kutokana na janga la Corona  walikuwa na fani   mbali mbali  zinatolewa  kwa muda mrefu (miaka 3) na muda mfupi (miezi 3 na 6) ni umeme wa majumbani na Viwandani (Electrical Installations), Nishati Jadidifu (Renewable Energy) Uungaji na Uundaji Vyuma (Welding and Metal

Fabrications),Upishi (Food Productions), Useremala (Carpentry and Joinery), Mitindo na Ushonaji (Design, Sewing and Cloth Technology), Ufugaji (Animal Husbandry), Uwashi(Masonry and Bricklaying), Mabomba (Plumbing and Pipe Fitting) na Kompyuta (Computer Applications).

MWISHO

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )