RC SINGIDA ATOA MAAGIZO MAZITO KUKAMILISHA UJENZI KITUO CHA AFYA CHIBUMAGWA

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni baada ya kukagua  ujenzi wa Kituo cha Afya cha Chibumagwa.
 Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Rahabu Mwagisa (kushoto) akiwa eneo kinapojengwa kituo hicho cha afya. Kulia ni Kaimu Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Ahmed Sulemani. 
 Mafundi wakiendelea na ujenzi wa kituo hicho.
Wananchi wakiwa eneo kinapojengwa kituo hicho cha afya.
Na Ismaily Luhamba, Manyoni

MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amewaagiza Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya Manyoni kusimamia kikamilifu ujenzi wa Kituo cha Afya cha Chibumagwa ili ukamilike kwa wakati.

Nchimbi ametoa agizo hilo mwishoni mwa wiki wakati alipotembelea kituo hicho kujionea hali ya ujenzi unavyoendelea.

“Nasema hivi hiki kituo nataka kiishe kwa muda ulio pangwa na serikali mpaka mwezi wa Julai muwe mmemaliza kila kitu na mwezi wa August 30 watu waanze kupata huduma hapa” alisma Dkt. Nchimbi.

Alisema Wananchi wana pata tabu na kwenda kutafuta huduma za kiafya zaidi ya kilometa 52 ndio maana serikali hii ya wanyoge imemua kutoa fedha ya kujenga kituo hicho ili kupunguza vifo vya mama na mtoto na wananchi kwa ujumla.

Katika hatua nyingine Dkt. Nchimbi amewataka wananchi wa eneo hilo kujitolea nguvu zao ili kituo hicho kikamilike kwa haraka.

Kwa upande wa Kaimu Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Ahmed Sulemani amemuhakikishia mkuu mkoa kuwa watamaliza ujenzi huo kwa wakati.

“Tunakuahidi kumaliza kazi hii kwa wakati na watu wetu ifikapo mwezi wa tisa wawe wanapata huduma hapa” alisema. Sulemani

Wanachi walikuwepo kwenye eneo la ujenzi wa Kituo cha Afya Chibumagwa wameishukuru Rais Dkt.John Magufuli kwa kuwa na moyo wa upendo hasa kwa kinamama kwa kuwajengea kituo cha afya.

“Tumefurahia sana tunamuombea kwa mungu azidi kuwepo madarakani kwani tunaona raha kula matunda ya nchi yetu “ alisema Veronica Hussein.

Kwaupande wake Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Chibumagwa, Saya Wambura alisema ujenzi wa kituo hicho ukikamilika utawarahishia utendaji wa kazi.

“Mkuu hapa kwenye hii zahanati yetu kwa sasa hatuwezi kutoa huduma za uzazi pingamizi kwa akina mama inatubidi tuwape rufaa ya kwenda Hospitali ya Wilaya ya Manyoni au kituo chochote cha jirani.” alisema Saya.

 Katika zahanati hiyo kwa mwezi wakina mama wanakwenda kujifungua ni 11 hadi 15 na ujenzi wa kituo hicho ukikamilika wajawazito wengi watakwenda kujifungua na kupata huduma  zote muhimu na hakutakuwa na sababu tena ya kumpoteza mama na mtoto. 
CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )