RC MNDEME AMPONGEZA MBUNGE MHE.KATAMBI KWA KUTOA MAJIKO YA GESI 600 KWA WAJASILIAMALI JIMBO LA SHINYANGA MJINI

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
amempongeza mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini ambaye pia ni Naibu waziri ofisi
ya waziri mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Mhe. Paschal Patrobas
Katambi kwa kutoa majiko ya gesi 600 ya kupikia kwa wajasiliamali wa Wilaya ya
Shinyanga.

Ametoa pongezi hizo Ijumaa Julai 21,2023 akiwa mgeni
rasmi kwenye hafla ya ugawaji majiko hayo ya gesi na kwamba hafla hiyo
imekwenda sanjari na semina ya kutoa elimu ya matumizi Bora kwa wajasiliamali
waliopokea majiko hayo.

RC Mndeme amesema majiko hayo yatawasaidia wananchi
hao kuepukana na uchafuzi wa mazingira unaotokana na utumiaji wa kuni pamoja na
mkaa wakati wa kupika.

“Asante sana Mhe. Mbunge kwa kutuletea majiko
haya rafiki kwa mazingira, sasa tutapika kwa wakati mfupi na urembo wetu utaongezeka
kwa sababu hatuchafuki tunakushukuru kwa kuwajali wananchi kata zote za Jimbo
la Shinyanga na niwaombe muende  mkatumie
majiko haya ya kisasa ili ndoa ziendelee kuimarika”
.amesema
Mndeme.

“Kati ya wabunge wanaofanya kazi vizuri,
Katambi yumo Katambi ni kijana mchapakazi na msikivu sana, mlifanya maamuzi
sahihi kumchagua mbunge huyu naomba tumuunge mkono, tusimkatishe tamaa, tumtie
moyo na tumuunge mkono kwa kumpa ushirikiano, huyu ni mtoto wetu tusitafute
mtoto mwingine”,
amesema RC Mndeme.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini
Mhe. Paschal Patrobas Katambi amesema ametoa majiko ya gesi zaidi ya mia tano
yenye thamani ya Shilingi Milioni 20.

Amesema lengo la kutoa majiko hayo ni kuwaepusha
wananchi na athari zitokanazo na matumizi ya mkaa pamoja na Kuni wakati wa
kupika chakula ambapo amesema ataendelea kutoa majiko ya gesi kwa
makundi mbalimbali ya wananchi katika jimbo lake.

“Nimefanikiwa
kugawa majiko haya kwa neema ya Mungu kwa kushirikiana na Kampuni ya Oryx
nimechukua mitungi zaidi ya Mia tano yenye thamani ya Shilingi Milioni 20 ili
ikasaidie wananchi wa Shinyanga lakini natarajia pia kuja kugawa awamu ya pili
kuweza kuhakikisha kwamba tunaunga mkono takwa la ilani ya chama cha mapinduzi
la kuhakikisha tunatunza mazingira kwa kumtua mama kuni kichwani”.
amesema
Mhe. Katambi

Aidha Mhe. Katambi amemshukuru  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea
kutoa fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta
ya  maji, elimu, afya, barabara na sekta
zingine kwenye jimbo lake ya Shinyanga mjini.

Mhe. Katambi ametumia nafasi hiyo amewataka wananchi wa jimbo hilo
kuwapuuza baadhi ya watu wanaopotosha kuwa Bandari ya Dar es salaam na Nchi
imeuzwa ambapo amesema  serikali ina nia
njema ya kufanya uwekezaji kwenye bandari ili kuongeza tija kwa ajili ya
maendeleo ya Taifa.

Baadhi ya wajasiliamali Wilaya ya Shinyanga waliopokea
mitungi hiyo Wameshukuru huku wakiahidi kuitumia vizuri majiko hayo ili
kuendelea kuwanufaisha.

Mbunge wa jimbo la Shinyanga Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Paschal Patrobas Katambi  ametoa
msaada wa Majiko 600 ya Gesi yenye thamani ya shilingi milioni 20 kwa
wajasiriamali wakiwemo wauza kahawa, mama lishe na baba lishe pamoja na makundi
mbalimbali ya wananchi katika jimbo hilo lenye jumla ya kata 17
kwa
lengo la kuwaepusha wananchi na athari zitokanazo na matumizi ya mkaa pamoja na
Kuni wakati wa kupika chakula huku akisema ataendelea kutoa majiko ya
gesi kwa wananchi wake.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini ambaye pia ni Naibu
waziri ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Mhe. Paschal
Patrobas Katambi akizungumza kwenye hafla yake ya kugawa majiko ya gesi
iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano jengo la CCM Mkoa wa Shinyanga.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini ambaye pia ni Naibu
waziri ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Mhe. Paschal
Patrobas Katambi akizungumza kwenye hafla yake ya kugawa majiko ya gesi
iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano jengo la CCM Mkoa wa Shinyanga.

Hafla ya kukabidhi majiko ya gesi yaliyotolewa na mbunge wa jimbo la Shinyanga Mhe. Paschal Patrobas Katambi kwa wajasiliamali mbalimbali wakiwemo mama lishe, baba lishe na wauza kahawa ikiendelea katika ukumbi wa mikutano jengo la CCM Mkoa wa Shinyanga.


CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )