Rais Magufuli Azindua Mradi Mkubwa Wa Maji Wa Kibamba-kisarawe Mkoani Pwani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanua Dkt John Pombe Magufuli amezindua mradi wa maji  wa Kibamba Kisarawe uliotekelezwa na Mamlaka ha Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA.


Mradi huo umejengwa  kufuatia agizo alilotoa Juni 21,2017 wakati wa uzinduzi wa Mtambo wa Ruvu Juu akiwataka Dawasa kutanua mtandao wa Usambazaji maji na kupeleka maji Kisarawe.

Akitoa maelezo ya mradi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema mradi wa Kisarawe umejengwa kwa fedha za ndani Bilion 10.6  zinazotokana na makusanyo ya maduhuli ya mauzo ya maji.

Luhemeja amesema wakati wa utekelezaji wa mradi huo, Dawasa iliona fursa ya kujenga mradi mwingine wa Bilion 7.3  wa kuyatoa maji katika tenki la Kisarawe linalohifadhi maji Lita Milioni 6  kupeleka katika maeneo ya Dar es Salaam.

Amesema, kukamilika kwa mradi wa maji Kisarawe  umewezesha maunganisho mapya  yapatayo 1650  na bado wanaendelea kufanya maunganisho mapya  na wananchi wanaendelea kupata maji safi.

Aidha, maeneo yatakayonufaika na mradi huo ni Kata za Kisarawe, Kazimzumbwi, Kiluvya, Kwembe, Kisopwa, Mloganzila na maeneo maalumu ya Viwanda.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )