RAIS MAGUFULI AMEMTENDEA HAKI MWLM.NYERERE NA WANA MARA-KHERI JAMES.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa na mlezi wa Mkoa wa Mara Komred Kheri James, amempongeza Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kazi kubwa aliyoifanya Mkoani Mara kwa kuendeleza ndoto ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kamabarage Nyerere ya kujenga hospitali ya Kwanga, ambayo ujenzi wake ulisimama tangu mwaka 1975, lakini sasa serikali ya Awamu ya Tano imetengewa fedha za kutosha na ujenzi wake unaendelea vyema sana.


Sambamba na hilo, Komredi Kheri amepongeza pia Ukarabati mkubwa wa shule ya Mwisenge alio somea Baba wa Taifa.Pamoja na pongezi hizo, Ndugu Kheri James ameeleza kuridhishwa na jitihada za serikali katika kuboresha Miondombinu, Huduma za afya, Mazingira bora ya Biashara na Uchimbaji madini wenye tija.


Komred Kheri James yupo mkoani Mara kwa ziara ya ukaguzi wa Miradi ya maendeleo ktk wilaya zote za mkoa huo.


Ziara hii imehudhuriwa na viongozi wa chama wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mkoa Ndg Samuel Kiboye, pamoja na viongozi wa serikali wakiongozwa na kamisaa wa chama Mh.Rc Adam Malima.


Katika ziara hii, Mlezi wa Mkoa amewasisitiza wana Mara kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa vitendo, na amewahimiza kuwa Wamoja ili kuchochea shughuli za uzalishaji maendeleo kwa ujumla.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )