PROF. MBARAWA AREJESHA FOMU YA URAIS CCM-ZANZIBAR

NA ANDREW CHALE, ZANZIBAR.

WAZIRI wa Maji wa Serikaliya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniaa, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa asubuhi ya leo 26 Juni, amerejesha fomu za kutaka kuteuliwa nafasi ya Mgombea wa Urais wa Zanzibar ndani ya Chama Cha Mapinduzi  (CCM) huku akisema kuwa Mwenyezi Mungu atabariki na atawezesha.

Prof. Makame Mbarawa anakuwa Kada wa 14 leo kurejesha fomu ambapo aliwasili majira ya saa nne Asubuhi na kisha kuhakikiwa kwa fomu zake na baadae kukabidhi  kwa Katibu wa Idara ya Organization CCM-Zanzibar, Cassian Galos.

Prof. Mbarawa alipongeza uongozi kwa kusimamia  utaratibu wa Chama kwa  kuwezesha wagombea wote  kupata wadhamini katika mikoa mitatu kati ya Unguja na Pemba.

Ambapo kila mgombea anatakiwa kupata wadhamini wasiopungua 250 ama zaidi.

“Nawashukuru viongozi wetu wa chama kwa kusimamia mchakato huu kwa umakini mkubwa.

Niwaombe tena kama nilivyosema siku ile nilipochukua fomu kuwa muniombee… ndugu zangu muendelee kutuombea Mwenyezi Mungu atafanya wepesi.” Alisema Prof. Mbarawa.

Mwenyezi Mungu atabariki, atawezesha na nyie ndugu muendelee kutuombea” alimalizia Prof. Mbarawa.

Hadi kufikia sasa tayari Makada wengine waliorejesha ni:

Balozi Ali Karume, Mohammed Hija Mohammed, Mbwana Bakari Juma,  Abdulhalim Mohammed Ali, Hamis Musa Omary.

Pia wamo Dk. Hussein Mwinyi, Mbwana Yahaya Mwinyi, Mohammed Jafary Jumanne, Dk. Khalid Salum Mohammed,  Rashid Ali Juma.

Pia wamo; Mmanga Mjengo Mjawiri, Bakari Rashid Bakari na Shamsi Vuai Nahodha.

MWISHO.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )