PROF. MAKAME MBARAWA, MWANAMAMA MWATUM SULTAN WAJITOKEZA KUCHUKUA FOMU ZA URAIS CCM ZANZIBAR

NA ANDREW CHALE, ZANZIBAR.

WAZIRI wa Maji wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniaa, Profesa Makame Mbarawa asubuhi ya leo 19 Juni, amechukua fomu za kutaka kuteuliwa nafasi ya Mgombea wa Urais wa Zanzibar ndani ya Chama Cha Mapinduzi  (CCM).

Makame Mbarawa anakuwa Kada wa 10 leo kuchua fomu baada ya jana 18 Juni Makada 9 kuchukua fomu.

Baada ya tukio hilo la kuchukua fomu, Makame hakuwa tayari kuongea na Wanahabari.

Aidha, kwa mara ya kwanza Kada wa CCM, Mwanamama, Mwatum Mossa Sultan  nae amejitokeza na kuchukua fomu na kufanya kuwa Kada wa 11 kwa waliojitokeza.

Mwanamama huyo alipata fursa ya kuongea na wanahabari ambapo amesema lengo ni kuongeza hamasa kwa akina mama wengine nao wajitokeze.

“Namuomba Mungu anipe subra. Aniongoze katika safari yangu hii ndefu.
Mimi ni Kada wa CCM na njna uzoefu mkubwa katika chama.” Alisema Mama Mwatum.

Wengine waliokwisha kuchukua fomu Afisi Kuu ya CCM-Zanzibar zilizopo Kisiwandui, Mjini hapa.

Ni pamoja na  Shamsi Vuai Nahodha, Mohammed  Jafari Jumanne, Mohammed Hija Mohammed.

Pia wamo Balozi Meja Jenerali Mstaafu, Issa Suleiman Nassor,
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,  Dk. Hussein Mwinyi aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Kwahani Mjini Unguja, Zanzibar.

Pia Mbwana Bakari Juma, Balozi Ali Karume, Mbwana Yahaya Mwinyi na Omary Sheha Mussa.

Tukio la kukabdhiwa fomu linatarajiwa kufungwa rasmi 30 Juni huku likisimamiwa na Katibu wa Idara ya Organization CCM, Zanzibar, Cassian Galos.

MWISHO.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )