PICHA: Mazishi ya Askofu Getrude Rwakatare yafanyika katika eneo la Kanisa la Mlima wa Moto lililoko Mikocheni B, Jijini Dar Es Salaam.

Mwili wa Mchungaji wa Kanisa la Mlima wa Moto, Mikocheni B, Assemblies of God, Askofu Dkt Getrude Rwakatare, umekwishapumzishwa katika nyumba yake ya milele, katika viunga vya kanisa hilo, jijini Dar es Salaam.


Mazishi hayo yamefanyika Alhamisi ya leo ya Aprili 23, 2020, majira ya saa 7:00 mchana na kuhudhuriwa na watu kadhaa ndani ya familia.Mama Rwakatare alifariki Dunia Aprili 20, 2020, katika hospitali ya Rabininsia, alikokuwa akipatiwa matibabu, ambapo kwa mujibu wa mwanaye Mutta Rwakatare, alisema kuwa Mama yao alikuwa akisumbuliwa na tatizo la moyo na presha.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )