OXFAM TANZANIA LANOA WATAALAM WA AFYA,WAZEE WA KIMILA VITA YA CORONA.

Msimamizi wa miradi Shirika la Oxfam Tanzania kanda ya kaskazini  Donath Fungu akiendesha mafunzo ya kuwajengea uelewa washiriki kutoka wilaya ya Hanang’,Babati,na maafisa sekta ya afya mkoa wa Manyara dhidi ya athari za virusi vya corona na namna ya kujikinga 
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uelewa dhidi ya athari za virusi vya Corona na namna ya kujikinga ikihusishwa na maswala ya kijinsia na kazi za nyumbani yaliyoandaliwa na shirika la Oxfam Tanzania 

 Afisa Maendeleo ya jamii kutoka kata ya Kateshi wilayani Hanang’ akichangia mada katika mafunzo hayo ya siku moja yaliyoandaliwa na shirika la Oxfam katika wilaya ya Babati mkoani Manyara 

Msimamizi wa miradi Shirika la Oxfam Tanzania kanda ya kaskazini  Donath Fungu akisisitiza jambo kwa washiriki wa mafunzo hayo ya siku moja 
Naelijwa Mshanga Afisa miradi kutoka shirika la Oxfam Tanzania kanda ya kaskazini akifuatilia mafunzo yanayoendelea  ya dhidi ya kujengewa ueklewa dhidi ya athari za virusi vya Corona na namna ya kujikinga ikihusishwa na maswala ya kijinnsia na kazi za nyumbani

 Msimamizi wa miradi Shirika la Oxfam Tanzania kanda ya kaskazini  Donath Fungu akihitimisha mafunzo ya kuwajengea uelewa washiriki kutoka wilaya ya Hanang’,Babati,na maafisa sekta ya afya mkoa wa Manyara dhidi ya athari za virusi vya corona na namna ya kujikinga 

 Mzee wa kimila Thomas Madiye Sixista akiwa na mkalimani wake Albert Masuja akielezea namna wao wanavyoshiriki katika kutoa elimu kwa jamii namna ya kujikinga na maambukizi ya uvirusi vya corona 

 Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakifuatilia kwa makini mafunzo yanayoendelea kutolewa

 Muendelezo wa mafunzo ya uelewa juu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kwa watendaji wa vijiji na kata pamoja na wazee wa kimila ,watumishi wa Afya katika mkoa wa Manyara 

Daktari Giliad Zablon kutoka hospitali ya wilaya Hanang’Tumaini akiainisha baadhi ya dalili za Covid- 19 kwa washiriki wa mafunzo ya kujengewa uelewa yaliyoandaliwa na kuendeshwa na shirika la kimataifa la Oxfam nchini Tanzania  

 Msimamizi wa miradi Shirika la Oxfam Tanzania kanda ya kaskazini  Donath Fungu akiendesha mafunzo ya kuwajengea uelewa washiriki kutoka wilaya ya Hanang’,Babati,na maafisa sekta ya afya mkoa wa Manyara dhidi ya athari za virusi vya corona na namna ya kujikinga 

Mmoja ya wazee wa kimila aliyehudhuria mafunzo hayo ya siku moja ya kujengewa uelewa dhidi ya athari za virusi vya corona na namna ya kujikinga.
Na.Vero Ignatus,Manyara
Oxfam Tanzania imeendesha Mafunzo ya kujenga uelewa dhidi ya athari za virusi vya corona na namna ya kujikinga ikihusishwa na maswala ya kijinsia na kazi za nyumbani na kuwahusisha watendaji mbalimbali kutoka yaliyofanyika Babati mjini ukumbi wa Good Life Hotel

Akizungumza Msimamizi wa miradi Shirika la Oxfam Tanzania kanda ya kaskazini  Donath Fungu amesema kuwa shirika hilo limetengeneza utaratibu kwaajili ya kukabiliana na majanga ,hivyo wameandaa mpango mkakati wa kujihadhari na kutambua ugonjwa huo una athari kiasi gani katika jamii na namna ya kukabiliana nao

Fungu amewataka viongozi wote walioshiriki mafunzo hayo kuhakikisha kuwa jamii kwa ujumla ambayo inahisiwa ipo   katika mazingira hatarishi wanakuwa na taarifa katika lugha ya kuaminika na taarifa hizo zitoke katika chanzo sahihi na kuepuka habari zinazoleta taharuki zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

 Daktari Giliad Zablon kutoka hospitali ya wilaya Hanang’Tumaini ameainisha baadhi ya dalili za Covid- 19 kuwa ni pamoja na homa, joto la mwili kupanda,mwili kuchoka,kupumua kwa shida,viungo kuuma,kichwa kugonga,mafua,kichefuchefu au kutapika,kuhara,vidonda vya koo,kikohozi wakati mwingine makohozi yanachanganyika na damu.
Amesema ni vyema kila mwanajamii ajenge tabia ya kunawa mikono marakwa mara kwa maji tiririka na waepuke kusalimiana kwa kushikana mikono pamoja na kukumbatiana

Kwa upande wake Katibu wa Afya mkoa wa Manyara Evance Simkoko amesema kuwa wameainisha sehemu maalum za kuwatenga wale wote wanaohisiwa kuwa na dalili za covid-19 kwaajili ya kuchukuliwa sampuli.

Simkoko  ameeleza juu ya serikali ya mkoa huo kudhibiti upandaji holela wa vitakatishi vya mikono pamoja nan doo zinazoandaliwa kwaajili ya maji ya kunawa katika maeneo mbalimbali.

Mafunzo hayo yamewashirikisha wenyeviti wa serikali za vijiji,wazee wa Kimila  wataalamu wa afya ,Maafisa maendeleo ya jamii wilaya Mafisa ustawi wa jamiii,pamoja na madaktari wa binadamu  ambapo waliendesha kikao hicho kwa njia ya majadala

Akizungumza kwa niaba ya wazee wa kimila Mzee Thomas Madiye Sixista amesema kuwa imekuwa ni changamoto kwa wazee hao kuifikia jamii kutoa elimu kutokana na kuzuiliwa kwa mikusanyiko ingawa wanaipongeza serikali kwa hatua walizozichukua na utoaji wa elimu unaoendelea katika jamii

Madiye amesema kuwa japokuwa elimu bado inahitajika kwani bado kwenye magari ya usafiri wa abiria  wameendelea kujaza abiria kupita uwezo wa gari

Aidha hadi sasa serikali imechukua jitihada mbalimbali za kuhakikisha wananchi wanajiepusha na maambukizi imeweka utaratibu kwenye viwanja vya ndege,kuzuia  vibali vya kusafiri nje yan chi, kufunga shule zote za msingi na vyuo,kuepuka mikusanyiko isiyokuwa ya lazima, kuhakikisha kuwa kila mwananchi ananawa mikono kwa usalama wake.

Ugonjwa huu wa Corona ulitangazwa kuingia nchini kwa mara ya kwanza 16 machi 2020 hadi sasa Tanzania imeripotiwa kuwa na nwagonjwa wapo 13 katika mikao ya Arusha 2 Dar es salaam 8,Zanzibar 2 na Kagera 1 hadi sasa hakuna taarifa zozote za kifo kilichosababishwa na ugonjwa wa virus vya Corona.

MWISHO

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )