NHIF TANGA WATOA HUDUMA NJE YA OFISI KUKABILIANA NA CORONA

 MENEJA
WA Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu
kulia akiteta jambo na Mwenyekiti wa Mtaa wa Senkrani Mohon Singh
aliyefika kwenye ofisi zao kupata huduma za bima ambapo kwa sasa wanatoa
huduma zao nje ya ofisi ikiwa ni sehemu ya kupunguza mkusuanyiko na
kuweza kukabiliana na ugonjwa wa Virusi vya Corona ambao kwa sasa
unaitikisa dunia.

 MENEJA
WA Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu
kushoto akimsikiliza mmoja wa wateja wao leo wakati wakitoa  huduma nje
ya ofisi zao ikiwa ni sehemu ya kupunguza mkusuanyiko na kuweza
kukabiliana na ugonjwa wa Virusi vya Corona ambao kwa sasa unaitikisa
dunia.

 MENEJA WA Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akimsikiliza mteja wao kama alivyokutwa leo

 Huduma zikiwa zinaendelea kwenye ofisi za nje kama inayoonekana huku wateja wengine wakiwa foleni

Afisa Uanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Tanga Mrisho Mponela akiendelea na kazi nje ya ofisi zao

MFUKO
wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga imelazimika kuhamisishia ofisi
nje ili kuweza kutoa huduma kwa wananchi wanaokwenda ikiwa ni sehemu ya
kupunguza mkusuanyiko na kuweza kukabiliana na ugonjwa wa Virusi vya
Corona ambao kwa sasa unaitikisa dunia.

Blog ya Kijamii ya Msumba News ililishuhudia baadhi ya huduma zikitolewa nje ya ofisi na
wananchi wakiendelea kupata huduma mbalimbali ambapo Meneja wa NHIF
Mkoa wa Tanga Ally Mwakababu alikuwa akiongoza zoezi la kusikiliza
wateja.

Akizungumza na Meneja wa NHIF Mkoa wa Tanga Ally
Mwakababu alisema kwamba dhamira kubwa ni kuonyesha jamii juu ya kujali
na kupambana na ugonjwa wa Corona lakini pia kuwasiliana na wateja wao
kwenye eneo lenye nafasi kubwa kwenye hewa kuliko kufanya kazi kwenye
ofisi ambapo wanakuwa wamejifungia.

Alisema hapo kila mtu anakaa
kwenye nafasi yake kwa mita mbili na mita moja na nusu kati ya mtu na
mtu na mazingira salama na wanapata hewa nzuri kutokana viti kuwa
mbalimbali ili kuweza kuwafanya wateja kuwa kwenye mazingira mazuri
ikiwemo eneo ambalo watu wananawa mikono kwa kutumia sanitize ambayo
kila anakuja kuhudumiwa anapatiwa.

Alisema kwamba wao kama mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya ni kiio kwa na kuonyesha kuitikia mwito wa
serikali kupitia Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na
Watoto Ummy Mwalimu kwamba suala la ugonjwa wa Corona sio la utani tena
ni lazima lichukuliwe kwa umakini mkubwa.

“Hivyo kutokana na
hilo na ndio maana tumeamua kutoa ofisi nje kwa lengo la kuweza
kuwasiliana na wateja wetu kwenye eneo kubwa na kila mtu anakaa kwa
nafasi kwa mita mbili au moja na nusu lakini mazingira salama huku kila
mtu anayekwenda kuhudumiwa lazima anaweze kunawa mikono kwa kutumia
Santinze”Alisema Meneja Mwakababu.

Hata hivyo alisema kwamba
pamoja na kuendelea kutoa huduma mbalimbali lakini eneo kubwa ambalo
wanalihimiza ni mpango wa toto afya kadi ambao unawawezesha watoto
kuweza kunufaika na matibabu pindi wanapokuwa wakiugua hivyo wameendelea
kulihamasisha kwenye maeneo mbalimbali.

Meneja huyo alisema
kwamba dhamira kubwa ya mfuko huo ni kuhakikisha inawafikia wananchi
wote kwenye maeneo mbalimbali mkoani Tanga ili waweze kujiunga nao na
hatimaye kuweza kunufaika na huduma za matibabu pindi wanapokuwa
wakiugua.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )