Ngasa: Tupo tayari kurejea kwenye ligi

MRISHO Ngasa, kiungo mkongwe ndani ya Klabu ya
Yanga amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya kurejea kwenye mechi za ushindani
baada ya kuanza mazoezi Mei 27.

Masuala ya michezo yalisimamishwa Machi 17 na
Serikali kutokana na janga la Virusi vya Corona ambavyo vinaivurugavuruga
dunia.Serikali imeruhusu masuala yamichezo kuanza Juni Mosi na tayari bodi ya
ligi imetangaza kuwa Juni 13 ligi itaanza.


Ngassa amesema kuwa wanaendelea vizuri na
mazoezi jambo linalowafanya wazidi kujiamini pale ligi itakapoanza.

“Kila kitu kinakwenda vizuri kwenye mazoezi na
kila mchezaji anafurahi kwani tulikuwa nje kwa muda mrefu, kwa sasa tupo tayari
kurejea uwanjani ili kuendelea pale ambapo tuliishia,” amesema.

Yanga ikiwa imefunga mabao 31, Ngasa amehusika
kwenye mabao matatu, akifunga mawili na kutoa pasi moja ya bao.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )