NANENANE DODOMA KUANZISHA MAONESHO YA KIMATAIFA YA UTALII WA MIFUGO

Mwakilishi wa Wakuu wa Mikoa ya Singida na
Dodoma  kwenye  Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kati, ambaye  pia ni 
Mkuu ya Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi 
Athuman Mukunda akijaribu 
kuendesha Trekta kwenye maonesho hayo 
leo, aliye pembeni yake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,
Prof. Elisante Ole Gabriel,  walio
chini  mwenye miwani ni Katibu Tawala
Mkoa wa Singida Dkt. Anjelina Lutambi na Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Injinia
Jackson Masaka wakishuhudia tukio hilo. Picha na John Mapepele
Mfugaji wa Mifugo Juma Seleman kutoka  Mpwapwa akipitisha Ng’ombe wake  Mashindano maalum ya Paredi ya mifugo iliyofanyika
kwenye maonesho ya nanenane kanda ya kati kwenye viwanja vya Nzuguni jijini
Dodoma. Picha na John Mapepele
Viongozi kutoka Mkoa wa Dodoma na Singida  pamoja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye
picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa 
mashindano maalum ya Paredi ya mifugo iliyofanyika kwenye maonesho ya
nanenane kanda ya kati kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma. Picha na John
Mapepele

Wawakilishi wa
Wakuu wa Mikoa ya Singida na Dodoma 
kwenye  Maonesho ya Nanenane Kanda
ya Kati,ambaye ni  Mkuu ya Wilaya ya
Bahi, Mwanahamisi  Athuman Mukunda(mwenye
kilemba) akimuuliza maswali muoneshaji wa kampuni la uzalishaji wa chakula cha
mifugo ya Harsho Group, Juma Ally (mwenye Tisheti ya Njano) Kulia ni Katibu
Tawala Mkoa wa Singida Anjelina Lutambi. Picha na John Mapepele
Na John mapepele, Dodoma

Wakuu wa Mikoa ya Dodoma na Singida wameiomba Serikali kupitia Wizara ya
Maliasili na Utalii  kuyafanya mashindano
maalum ya Paredi ya Mifugo yanayofanyika kila mwaka kwenye  kanda ya kati kwenye viwanja vya Nzuguni  jijini Dodoma kuwa Maonesho ya Kimataifa  ya utalii wa mifugo ili kuongeza pato la
taifa na kuleta hamasa kwa wananchi kushiriki.

Katika hotuba iliyotolewa kwenye Paredi la Mifugo leo na Mkuu ya Wilaya
ya Bahi Mwanahamisi  Athuman Mukunda kwa
niaba ya Wakuu hao wa Mikoa, amesema Tanzania imebarikiwa kuwa nchi ya
pili  kwa kuwa na mifugo mingi barani
Afrika  hiyo uanzishaji uboreshaji wa Paredi
 la mifugo utasaidia  kuinua uchumi wa taifa kwa kuongeza  kipato kutoka kwa watalii  kupitia mifugo.

Ameongeza kuwa jiografia ya Dodoma kuwa katika ya nchi na  hali ya hewa nzuri ya majira ya mwezi Agosti
katika eneo la Nzuguni  linafanya watalii
wengi kuja kutembelea maonesho hayo.

“Ndugu zangu  niwaambie ukweli  katika nchi yetu miongoni mwa Wizara mama
ambazo ni nguzo na tegemeo wa maisha ya wananchi wake na ambayo inaweza
kuongeza mapato ya Serikali ni  Wizara ya
Mifugo na Uvuvi”  alisisitiza Mhe.
Mukunda

Amesema mifugo na uvuvi ni dhahabu inayotembea ambayo kama  itatunzwa 
kwa kuzingatia ushauri na utaalam 
utaongeza tija na kulifanya taifa lisonge  mbele 
kiuchumi

Hata hivyo amesema changamoto inayosababisha kutokuwa na mageuzi ya
haraka kwenye Sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi nchini ni kukosekana kwa wataalam
kwenye  ngazi za chini kwa wananchi
ambapo amesisitiza kuwa  kuna umuhimu
Wizara husika kushusha wataalam hadi kwenye ngazi za vijiji  badala yahali ilivyo sasa ambapo wataalam  wapo kwenye ngazi za juu jambo ambalo
linafanya utalaamu usiwafikie wananchi kama ilivyokusudiwa.

Aidha ameongeza kuwa kuna haja ya Wizara husika kuboresha ushirikiano
katika utekelezaji  na utoaji wa
maelekezo ambapo amesema  kumekuwa na
ushahidi kuwa sehemu ambazo wizara zimeshirikiana kikamilifu na Halmashauri
husika kumekuwa na matokeo chanya.

 Naye Katibu Tawala Mkoa wa
Singida Dkt. Anjelina Lutambi amepongeza Rais John Pombe Magufuli kwa kazi
kubwa anayoifanya kwenye Sekta mbalimbali hapa nchini ikiwa ni pamoja na
Kilimo, Mifugo na Uvuvi ambapo ameelekeza 
Halmashauri za Mkoa wa Singida kutenga maeneo  kwa ajili ya kulima malisho ya  mifugo na ameishukuru Wizara ya Mifugo kwa
kushirikiana na Halmashauri ya Ikungi kuanzisha shamba darasa  bora la malisho ya mifugo ambalo ni la mfano
hapa nchini.

“Ukiona Mheshimiwa, Rais Dkt. John Magufuli anawekeza kwenye miradi kama
ule wa kufua umeme wa Mwalimu Nyerere Rufiji, Reli ya kisasa kutoka Dar es
Salaam hadi Makutupola ya Singida lengo ni kujenga uchumi jumuishi” ameongeza
Dkt. Lutambi

Amesema Mkoa wa Singida umendelea kupiga hatua katika kutekeleza   miradi mbalimbali ambapo amesema licha ya
kufanya mapinduzi makubwa kwenye zao la Korosho   pia wamesimamia  vizuri sekta nyingine  kama vile 
sekta ya madini ambapo muelekeo wa sekta ya madini ni kuwafanya wananchi
wamiliki raslimali hii kwa kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi. Mheshimiwa Luhaga Joelson Mpina amesema  Serikali 
ya awamu ya Tano imefanya mageuzi makubwa  kwenye sekta ya mifugo ambapo  viwanda vingi vya nyama  vimeanzishwa, kuboresha kwa miundombinu ya
mifugo kama majosho na kuimarisha 
minada, kuzuia utoroshaji wa 
mifugo kwenda nchi jirani na 
kuanza  kutengeneza  chanjo za mifugo ambapo hadi sasa chanjo sita
zimekamilika na  nyingine saba
zinatarajia kukamilika katika kipindi 
kifupi kijacho na kufanya 
chanjo  dhidi ya magonjwa 13 za
kipaombele kukamilika.

Aidha, amesema Wizara  ya Mifugo
tayari imeshatangaza  rasmi tarehe
13/5/2020  bei elekezi za chanjo za
wanyama dhidi ya magonjwa 13 ya kipaombele 
kwa mujibu wa Sheria ya Magonjwa ya Wanyama Na. 17 za Mwaka  2020 kifungu cha 3(2)(g) na Kanuni za Chanjo na
Uchanjaji Na 180 za Mwaka 2020 Kifungu cha 14(b) na (c)  ambapo bei ya dukani nay a kuchanjia kwa dozi
 haitazidi  viwango vilivyoainishwa.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )