NAIBU WAZIRI SILINDE ASHITUKIZA KATIKA SHULE ZA TUMAINI NA MILADE SINGIDA

 Naibu waziri wa TAMISEMI David Silinde amefanya ziara ya kushtukiza katika shule za Tumaini sekondari iliyopo wilaya ya Iramba na shule ya msingi Milade iliyopo wilaya ya mkalama mkoani Singida kufatilia maagizo yake aliyoyatoa mwezi December 2020.


Naibu waziri Silinde ameridhishwa na ujenzi wa madarasa,mabweni na bwalo katika shule ya sekondari ya Tumaini iliyopo wilaya ya Iramba mkoa wa Singida baada kupita kukagua ujenzi huo mwezi deember na kutoridhishwa na ujenzi huo na kuagiza ukamilike ndani ya mwezi huu wa pili.

Naibu waziri Silinde ameshitukiza katika shule hiyo kukagua ujenzi huo akitokea Mwanza katika msiba wa Aliyekua katibu Tawala mkoa wa Arusha Richard Kwitega.

Aidha itakumbukwa Naibu waziri Silinde aliagiza kuondolewa kwa mkuu wa shule hiyo na kuvunja kamati ya ujenzi wa shule hiyo baada ya kukuta kusuasua kwa ujenzi huo ikiwa serikali imeshapeleka fedha zote za ujenzi katika akaunti shule lakini usimamizi ulikua mdogo lakini sasa ameridhika baada ya ujenzi kufikia pazuri na kumwahidi mpaka tarehe aliyoitoa ujenzi utakua umekamilika.

Wakati huohuo naibu waziri Silinde alitembelea kukagua maagizo yake ya kukamilisha ujenzi katika shule ya msingi Milade iliyopo wilaya ya mkalama na kukuta wamekamikisha ujenzi na kuridhika na ujenzi huo na kuagizo shule zote ambazo walipata fedha za miradi ya lipa kwa matokeo EP4R wamalize ujenzi haraka kwani hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa kwa wale ambao watashindwa kukamilisha ikiwa wameshapitisha mda waliotakiwa kukamilisha miradi hiyo ambayo ni mwezi Desemba mwaka jana.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )