NAIBU WAZIRI NYONGO AONGOZA KIKAO CHA MARIDHIANO NA KUPOKEA OMBI LA MWEKEZAJI

NAIBU
Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akisaini kitabu cha wageni mara baada
ya kuwasili kwenye ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Nzega ili kusikiliza
maombi na kutatua  changamoto za wachimbaji wadogo wa madini Aprili 27
mwaka huu

NAIBU
Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo kulia akihoji jambo kwa wachimbaji
waliokuwa wakilalamika kutopewa leseni kwenye eneo ambalo waliliomba
jambo ambalo RMO alipaswa kukaa na pande hizo kutafuta muafaka
NAIBU
Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akizungumza na waandishi wa habari
juu ya makubaliano yaliyofikiwa mara baada ya wajumbe kujadili maombi ya
mwekezaji ya kutaka kupunguziwa gharama ya ununuzi wa madini ya dhahabu
baada ya uchenjuaji wa marudio wa mchanga wa dhahabu ulioachwa na
mwekezaji mkubwa wa madini wa kampuni ya  Resolute iliyokuwa ikifanya shughuli zake wilaya ya Nzega kufunga mgodi

NAIBU
waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Nzega
kulia Godfrey Nyapula wakati wa kikao na wachimbaji wadogo wa madini
kilichofanyika kwenye ofisi za Mkuu huyo wa wilaya Aprili 27 mwaka huu
KATIBU
Mtendaji wa Tume ya Madini Proffesa Shukrani Manyaa akizungumza na
waandishi wa habari juu ya hatua zinazofuata baada ya kikao cha kuridhia
ombi la mekezaji ili utekelezaji wake uwekwe katika utaratibu
unaokubalika kisheria

Naibu Waziri wa Madini,
Stanslaus Nyongo, akiongoza kikao kilichohudhuriwa na Katibu Mtendaji wa TumeyaMadini,
Prof. ShukraniManya, MkuuwaWilayayaNzega, Godfrey Ngupula,
Afisa  Madini Mkazi wa Mkoa waTabora, Mhandisi Mayingi Makalobela, Mkuu wa Chuo cha
Nzega, Nuru
Shaban Kamati ya Ulinzi na Usalama  wilaya ya Nzega pamoja na mwekezaji wa uchenjuaji wa marudio,
RashedShabout Said.

Afisa Madini Mkazi wa Mkoa waTabora,
Mhandisi Mayingi Makalobela akitoa maoni yake juu ya ombi la mwekezaji Rashed Shabout
Said wa uchenjuaji wamarudio ya mchanga ulioachwa na kampuni ya resolute
baada ya mgodi huo kufungwa.

SERIKALI 
imeridhia ombi la kupunguza gharama ya ununuzi wa dhahabu unaofanywa na
mwekezaji Rashed Shabout Said wa kampuni ya Ashery Construction
&Matinje gold Extraction yauchenjuaji wa marudio ya mchanga wa
dhahabu ulioachwanakampuniya Resolute iliyofunga shughuli zake za
uchimbaji mkubwa wa madini ya dhahabu mwaka 2014.

Makubaliano
hayo yalifikiwa Aprili 27, 2020 wakati wa kikao kilichoongozwa na Naibu
Waziri wa Madini, Stanslaus  Nyongo kilicholenga kujadili ombi la
mwekezaji Rashed Shabout Said anayechenjua dhahabu kwenye mabaki hayo ya
mchanga wa dhahabu ulioachwa na kampuni ya Resolute iliyokuwa ikichimba
dhahabu wilayani Nzega,MkoaniTabora.

Pamoja na NaibuWaziri
Nyongo kikao hicho kiliwahusisha Katibu Mtendaji wa Tume ya
Madini,Profesa Shukrani Manya, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tabora
Mayingi Makalobela, Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Godfrey Ngupula, Mkuuwa
Chuo cha Madini kampasi yaNzega, Nuru Shabani, Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Wilaya ya Nzega pamoja na  ujumbe ulioambatana na mwekezaji
huyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao
hicho, Naibu Waziri Nyongo alisema, kikao kimeridhia ombi moja kati ya
matatu yaliyowasilishwa na mwekezaji ikiwa ni kushusha bei ya kumwuzia
dhahabu kiasi kilichopunguzwa kimsaidie kulipia  gharama nyingine
anazozitumia katika uwekezaji huo.

Nyongo alisema Rashed aliomba
kupunguzi wa gharama ya dhahabu anayoinunua serikalini mara baada ya
uchenjuaji, kuondolewa gharama za watumishi wanaoshiriki katika
kusimamia mchakato mzima wa uchenjuaji wa mchanga huo pamoja na
kuondolewa malipo ya mrabaha nakurudishiwa pesa zilizolipwa kama mrabaha
kwa awali mbili za uchenjuaji zilizopita.

Nyongo alibainisha
kuwa Wizara kwa kushirikiana na Tume ya madini zimeridhia kupunguza
gharama ya kuuza dhahabu kwa  mwekezaji huyo na kwamba huduma nyingine
na malipo ya mrabaha yatapaswa kulipwa kama kawaida  kwa mujibu wa
sheria.

Kwaupande
wake, KatibuMtendajiwaTumeyaMadini, Prof. Shukrani Manya alisema ombi
la mwekezaji limepokelewa na kwamba hatua inayofuata nikwenda kupitia na
kurekebisha mkataba ikiwani pamoja na kupeleka maoni yaliyofikiwa na
kikao hicho kwa mamlaka nyingine ili kumwezesha mwekezaji huyo kufanya
kazi yake kwa tija na bila manung’uniko.

Akizungumza na
waandishi wa habari mwekezaji Rashed, aliishukuru serikali kwa kupokea
na kufanyia kaziombi lake na kukiri hakutegemea kuwa angesaidiwa kw
aharaka namna ilivyofanyika nakukiri kwamba hakika Serikali ya Awamu ya
Tano inasikilizana kutatua changamoto za wananchi.

“Nashukuru
sana kwa serikali hadi Naibu Waziri kuja kunisikiliza kwa kweli Wizara
ya madini nisikivu sana, nashukuru sana” Rashed alikazia.

Akizungumzia
changamoto wanazokutana nazo kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa corona
Rashed alisema kumekuwa na changamoto ya usafirishaji wa madini kutokana
na ndege nyingi za nje kusitisha safari zanje hivyo inakuwa ngumu kwa
kuendesha biashara.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )