NAIBU WAZIRI AWESO AZINDUA JUMUIA ZA WATUMIA MAJI MTO PANGANI CHINI ATOA ONYO JUMUIYA ZA MAJI

NAIBU
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jumuiya za
Watumia Maji Mto Pangani chini uliofanyika kwenye viwanja vya Sokoni
wilayani Pagani
Mwenyekiti
wa Bodi ya Maji ya Bonde la Pangani Dkt Victor Runyoro akizungumza
wakati wa uzinduzi huo kushoto ni Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso na
kulia ni Mkurugenzi wa Bonde la Maji la Mto Pangani Segule Segule

 Mkurugenzi
wa Bonde la Maji la Mto Pangani Segule Segule akizungumza wakati wa
uzinduzi huo kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Bonde la Mto Pangani
Dkt Victor Runyoro kushoto ni Mwenyekiti wa Halamshauri ya wilaya ya
Pangani Seif Ally

 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Pangani Rajabu Abdallah akizungumza wakati wa uzinduzi huo

 KATIBU Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Mwalimu Hassani Nyange akizungumza wakati wa uzinduzi huo

 Naibu
Waziri wa Maji Jumaa Aweso  katikati akikata utepe kuashiria uzinduzi
wa Jumuiya ya Watumia Maji Mto Pangani chini na ugawaji wa vitendea kazi
kwa Jumuiya kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Bonde la Maji Mto Pangani
Dkt Victor Runyoro na kulia ni Mkurugenzi wa Bonde la Maji la Mto
Pangani Segule Segule

 
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akijaribu moja ya vitendea kazi
vilivyotolewa kwa Jumuiya ya watumia maji Mto Pangani chini wakati
alipoizindua

 Sehemu ya wananchi waliojitokeza kushuhudia uzinduzi huo

 Sehemu ya vifaa walivyokabidhiwa

NAIBU
Waziri wa Maji Jumaa Aweso amezindua Jumuiya ya watumiaji wa Maji Mto
Pangani chini wilayani Pangani huku akizitaka vifaa vilivyokabidhiwa kwa
ajili ya kufuatilia rasilimali za maji wasivitumie kama bodaboda na
kupakiza nazi badala yake vitumike kwenye matumizi yaliyokusudiwa.

Hayo
yalisemwa na Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso wakati wa uzinduzi wa
Jumuiya ya Watumiaji Maji wa Mto Pangani chini katika halfa iliyofanyika
mjini humo na kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Maji ya Bonde la
Pangani Dkt Victor Runyoro na Mkurugenzi wa Bonde la Maji la Mto Pangani
Segule Sugule.

Alisema kwamba kumekuwa na tabia jumuiya
zinapokabidhiwa vifaa kwa kufuatilia rasilimali za maji huacha kufanya
hivyo huku wakivitumia kwenye matumizi ambayo hayajakusudiwa huku akitoa
onyo kwao.

“Ndugu zangu mmekabidhiwa vifaa hivi ikiwemo
pikipiki hivyo niwatake isije kutokea bodaboda zikaenda kupakizwa nazi
na popoo na kuacha kutumika kwenye matumizi yaliyokusudiwa kwani kufanya
hivyo mtakuwa hamtendi haki na tutakaowabaini tutawachukulia hatua
“Alisema Naibu Waziri Aweso.

Hata hivyo alisema kwamba anaamini
vifaa hivyo ambayo vimetolewa vitakuwa chachu kubwa katika jumuiya hizo
kuhakikisha zinaweza kushughulikia changamoto mbalimbali.

Aidha
alisema kuanzishwa kwa jumuiya hiyo ni lazima wahakikishe wanatimiza
majukumu yao na waledi mkubwa ili kuweza kuongeza ufanisi wakati
wakitekeleza majukumu yao.

“Ndugu zangu wajibu wenu ni
kuhakikisha mnasimamia ipasavyo rasilimali za maji kutokana na uwepo wa
vitendea kazi hivyo mimi ni kijana wenu ikitokea mnafanya vibaya
tutaivunja na kutafuta watu wengine ambao wataweza kufanya kazi kwa
mujibu wa katiba iliyoasisiwa”Alisema

Hata hivyo aliwaambia
kwamba yeye ni kiongozi kutoka wilayani humo hivyo laqzima wahakikishe
wanakuwa jumuiya ya mfano hapa nchini kwa kufanya kazi kwa waledi
mkubwa. 

Awali
akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri Aweso Mwenyekiti wa Bodi
ya Maji ya Bonde la Pangani Dkt Victor Runyoro alisema bonde la Pangani
linasimamia wilaya 20 ambazo ni nyingi lakini kwa majukumu waliopewa
kisheria na kubwa ni kuhifadhi rasiliamali maji.

Alisema kwamba
maeneo mengi wanamatatizo ya maji wanapata shida sana na jinsi idadi ya
watu inavyozidi kuongezaka maji kwa mtu mmoja yanadizi kupungua.

Naye
kwa upande wake Mkurugenzi wa Bonde la maji la Mto Pangani Segule
Segule alisema suala la utunzaji wa maji ni jukumu lao kila mmoja
kuhakikisha rasilimali za maji vinatunzwa kwa ajili ya vizazi vya sasa
na vijavyo

Alisema uundwaji wa jumuiya hizo zinaundwa kwa
kuzingatia sheria za rasiliamali za maji ya namba 11 ya mwaka 2009
katika maelekezo ya sheria kuunganisha maelezo ya sera ya maji 2002
ambayo inataka ushirikishwaji jamii kwenye miradi na masula yote
yanayohusu maji.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )