NAIBU WAZIRI AWESO ATOA AGIZO KWA MAMLAKA ZA MAJI NCHINI

 NAIBU
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza wakati akifungua  mkutano wa
wadau wa mamlaka ya Maji na Usafiri wa Mazingira (Tanga Uwasa) wilaya ya
Pangani kulia Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly

 KATIBU
Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassan Nyange kulia akisistiza
jambo wakati wa mkutano huo kushoto ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa
Mhandisi Geofrey Hilly akifuatiwa na Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso

 Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga
Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo

 MENEJA
Ufundi wa Tanga Uwasa Mhandisi Rashid Shabani akieleza mkakati wa
kuboresha huduma za maji mjini Pangani wakati wa mkutano huo

  Kaimu Mkuu wa kitengo cha Huduma kwa Wateja Rogers Machaku

 Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye mkutano huo wa wadau

 MKURUGENZI
wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Isaya Mbenje akiwa kwenye meza kuu
na Mwenyekiti wa mkurano huo wa wadau kulia na wa kwanza kulia ni
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly

 NAIBU
Waziri wa Maji Jumaa Aweso kushoto akisalimiana na MENEJA Ufundi wa
Tanga Uwasa Mhandisi Rashid Shabani wakati alipowasili kufungua mkutano
huo katikati ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly

 Sehemu ya wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye mkutano huo wa wadau

Mmoja wa wananchi akiuliza swali katika mkutano huo

 Sehemu ya wadau mbalimbali wakifuatilia mkutano huo

 Sehemu ya wadau mbalimbali wakifuatilia mkutano huo

 Sehemu ya wadau mbalimbali wakifuatilia mkutano huo

NAIBU
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso ameziagiza mamlaka za maji nchini kuwa na
utaratibu wa kuwashirikisha wadau wanaotumia huduma za maji kwenye
maeneo yao.

Aweso aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wa
wadau wa mamlaka ya Maji na Usafiri wa Mazingira (Tanga Uwasa) wilaya ya
Pangani ambapo alisema ni muhimu wadau kushirikishwa.

Alisema
hilo linatokana na kwamba wao ni muhimu na ndio wenye maeneo yao hivyo
ni wajibu kuona namna ya kuwashirikisha badala ya kwenda tu bila wao
kutambua.

Aidha aliwapongeza Tanga Uwasa kwa kuwashirikisha
wahusika kwani moja ya makosa makubwa yanayofanywa na wataalamu wetu
licha ya kuwa na elimu kubwa lakini kosa kubwa wanalolifanya ni
kutokuwashirikisha wahusika.

“Ndugu zangu mtambue kwamba
anayelala na mgonjwa ndio anayejua muhimo yake leo mnaweza kuja na
magari na vifaa bila kuwashirikisha wadau mnaficha nini?…niwaombe
mshirikiana na hao viongozi hamtashindwa chochote kwani hata leo
pakitokea ubadhirifu watawapa taarifa “Alisema Naibu Waziri huyo.

“Leo huu ni mkutano wa wadau wa Tanga Uwasa Pangani niwapongeze Tanga
Uwasa kwa hatua hii muhimu lakini nitoe agizo kwa mamlaka za maji nchini
kuwa na utaratibu wa kuwashirikisha wadau wanaotumia huduma ya maji
kwenye maeneo yenu kwani wao ndio wenye maeneo yao na na sio kwenda tu
“Alisema Naibu Waziri Aweso.

Akizungumzia suala la bili za maji,
Naibu Waziri Aweso alisema ni wajibu na jukumu la wananchi kupatiwa
maji na mwenye jukumu hilo ni wizara ya maji kupitia mamlaka za maji.

Alisema
pamoja na jukumu hilo lakini wasisahau kwamba wananchi wana wajibu wa
kuhakikisha wanalipa bili za maji lakini zisiwe bandikizi ambazo
zitaleta manung’uniko kwao

“Kwamba
kama mtu leo anatumia maji ya elfu thelathini unamuambia alipe laki
mbili kama anakiwanda na ndio maana tukatoa agizo kwamba mnaposoma bila
za maji muwashirikishe wananchi husika”Alisema Naibu Waziri Aweso.

Pia
alisema wizara hiyo imefanya maboresho makubwa wanajua mji wa Pangani
watu wameongezeka ukilinganisha na kipindi cha nyuma tumepata mradi wa
milioni 500 umetengenezwa wananchi wanapata maji .

Hata hivyo
alisema yeye kama Mbunge wa Pangani kilio chake cha muda mrefu ni kuona
kwanini Mto pangani unapita katikati ya mji wa Pangani lakini haya maji
hayatumiki hicho ndio kilio kweli muosha huoshwa.

“Mh Rais
akanipa Wizara ya Maji naomba nizungumze kwa heshima na ujasiri mkubwa
tenda zaidi ya miji 24 miradi mikubwa na sisi Pangani tutatumia maji ya
Mto Pangani lakini utakwenda pia miji ya Muheza na Handeni na Korogwe
hata nikifa leo hii kumbukumbu haitasahauilika kwa kazi kubwa
aliyoifanya Rais wetu”Alisema Naibu Waziri huyo.

Hata hivyo
alisema kwamba mamlaka ya Maji ya Tanga Uwasa wamekuwa wakifanya vizuri
sana kila mwaka na ndio maana wakaona wawaunganishie na wilaya za Muheza
na Pangani.

Awali akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi wa
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga “Tanga Uwasa”
Mhandisi Geofrey Hilly alisema leo wapo Pangani kuongea na wadau wao
mbalimbali kwa ajili ya kuweka uelewa mpana kwanini wao wa Tanga Uwasa
wamekwenda kutoa huduma kwenye mji huo . 

Alisema
kwamba mji wa Pangani utaratibu wa sasa una kata nne una wakazi wapatao
19100 ambao wanapaswa kuwahudumia kwa hiyo wamepata viongozi wa ngazi
ya chini mpaka juu kuongea nao na wakiongea nao ni sawa na kuwafikia
wananchi.

Alisema wajue kwamba kwa nini Tanga Uwasa wanatoa
huduma huko huku akieleza hayo ni maamuzi ya Serikali kupitia Rais Dkt
John Magufuli ambapo mwaka 2017 alitangaza rasmi huduma za maji zote
zisimamiwe wizara ya maji.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )