NAIBU SPIKA BARAZA LA WAWAKILISHI BI. MGENI HASSAN JUMA ACHUKUA FOMU YA URAIS CCM-ZANZIBAR

NA ANDREW CHALE, ZANZIBAR.

NAIBU Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar,  Bi. Mgeni Hassan Juma  amekuwa Mwanamke wa Nne kujitokeza kuchukua fomu ya Urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi CCM Zanzibar.

Bi. Mgeni amewasili viunga Afisi Kuu ya CCM-Zanzibar eneo la Kisiwandui mjini hapa majira ya saa Tisa Alasiri akiwa na wapambe magari mawili na wapambe wake sita.

Baada ya kuchukua fomu hiyo alipata wasaha wa kwenda kuomba dua maalum katika kaburi la Hayati Abeid Aman Karume na kisha kupata fursa ya kuongea na Wanahabari

Bi. Mgeni alieleza kwa ufuoo ujio wake wa kuchukua fomi ni kutia moyo wanawake wengine kwani yeye ni miongoni mwa wanawake viongozi na wanaharakati wa Wanawake.

Nimesema nije kuwa miongoni mwa wenzangu 30 waliojitokeza kuchukua fomu hadi sasa na mimi 31 hii ni Demokrasia ndani ya Chama chetu.

Ujio wangu pia ni fursa kwa Wanawake wengine ilikutekeleza kauli mbiu kwa vitendo ya 50 kwa 50″ Alisema Bi. Mgeni.

Aidha, alisema kuwa amekuwa katika nafasi mbalimbali ikiwwmo Mashirika binafsi, Mwalimu Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi akwa vipindi tifauti ikiwemo kwa nafasi ya kundi la Wasomi na sasa pia ni Naibu Spika.

Bi Mgeni anaungana na makada wengine Wanawake ambao ni pamoja na Mwatum Mussa Sultan, Hasna Attai Masoud na Fatuma Kombo Masoud.

Mwisho.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )