Mwanamke wa Kwanza Ajitosa Kugombea Urais Zanzibar Kupitia CCM

Mwantum Mussa Sultan amechukua fomu ya kugombea Urais Zanzibar na anakuwa Mwanamke wa kwanza kujitosa kwenye kinyang’anyiro cha Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),


Mwantuma amechukua fomu Leo Ijumaa tarehe 19 Juni 2020 katika Ofisi za CCM visiwani Zanzibar zilizoko Kisiwandui na kukabidhiwa Cassian Gallo’s, katibu wa Kamati Maalumu ya NEC Idara ya Oganaizesheni Zanzibar.

Mara baada ya kukabidhiwa, Mwantumu amesema, amefanya hivyo ili kutoa hamasa kwa wanawake kujitosa katika kinyang’anyiro hicho, kutimiza sera ya haki sawa kwa wote.
 
Mwantumu anakuwa kada wa 11 wa CCM kujitosa katika kinyang’anyiro hicho, tangu zoezi hilo la siku 15 lifunguliwe Jumatatu ya tarehe 15 Juni 2020.
CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )