MTATURU : RAIS MAGUFULI KINARA WA MABADILIKO

MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu amesema mabadiliko ya kimaendeleo yaliyofanyika katika serikali ya awamu ya tano chini Rais Dkt John  Magufuli ni makubwa yanayopaswa kuenziwa na kubebwa na watanzania wote.

Mtaturu amesema hayo jijini Dodoma wakati akizungumzia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu iliyowasilishwa na kupitishwa katika bunge la 11 linaloendelea jijini Dodoma.

“Naomba niseme ukweli Rais Magufuli amefanya kazi kubwa,haya mambo yanahitaji utashi wa kisiasa, sisi wabunge tunatoka majimboni,ukiuliza mbunge mmoja mmoja ambavyo serikali imegusa maisha ya wananchi wa jimbo lake atakueleza sio chini ya mambo matatu,”alisema Mtaturu.

Amebainisha baadhi ya mambo yaliyofanyika kuwa ujenzi wa vituo vya afya zaidi ya 352 vimejengwa,umeme umesambazwa vijijini,elimu bila ya malipo na kuweka mazingira wezeshi ya kufanyia biashara kwa wajasirimali wadogo wadogo,

“Haya ni mapinduzi makubwa katika nchi yetu haijapata kutokea,sekta ya afya tangu Uhuru tulikuwa na na vituo vya afya 115 tu lakini leo ndani ya kipindi cha miaka minne tumepata vituo zaidi ya 352,haya ni mafanikio makubwa sana,

“Niseme hivi,tulimuamini 2015 na tumeona imani inaongezeka zaidi kutokana na miradi mingi kutekelezwa,hivyo 2020 tusimame nae ili aendelee kuipaisha nchi yetu kimaendeleo zaidi,”aliongeza Mtaturu.

Mwisho.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )