Mrema aongoza chama chake kwa kutumia WhatsApp


Mwenyekiti wa Chama cha TLP Augustino Mrema, amesema kuwa kwa sasa amekubaliana na viongozi wenzake, kufanya mazungumzo yote yanayohusu chama kupitia makundi mbalimbali ya WhatsApp waliyoyaunda ikiwa ni tahadhari ya Virusi vya Corona.

 Mrema amesema kwa sasa yeye hatoki kabisa nje mara nyingi amekuwa akibaki ndani na wajukuu zake na kutoa msisitizo kwa watu wengine pia, kama hawana sababu zozote zinazowafanya watoke nje ni bora wabaki nyumbani.

“Kwa sasa mimi sifanyi mienendo isiyo ya lazima, kama ni ofisi tumekubaliana na Katibu Mkuu kuna mambo yeye anaweza kuyafanya, Mei 5 tutakuwa na Mkutano Mkuu kwa ajili ya kumpitisha Rais Magufuli kuwa mgombea wa chama chetu, kwahiyo mawasiliano yote tunayafanya kwa njia ya makundi ya WhatsApp” amesema Mrema.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )