MKUU WA WILAYA YA MONDULI AIPONGEZA ALAT MKOA WA ARUSHA

Mkuu wa wilaya ya Monduli Ameipongeza ALAT Mkoa wa Arusha kwa usimamizi mzuri  katika kusimamia Halmashauri zote katika mkoa wa Arusha kwani  kumekuwa na utekelezaji Mkubwa katika Miradi ya Maendeleo katika  Halmashauri zote za Mkoa wa Arusha.
.
.
.
Mkuu wa wilaya Monduli  amesema hayo alipokuwa akihutubia Kikao cha Mwisho cha ALAT ambapo wanahitimisha Miaka mitano katika kusimamia Halmashauri zote katika kutekeleza majukumu  Mbalimbali.

Dc Kimanta   amewapongeza Waheshimiwa Madiwani ambao ni wajumbe wa Kamati ya ALAT kwa kuondoa  tofauti zao na  kuweka Maslahi mbele  ya kuwahudumia wananchi na kwakuwaletea  maendeleo.Amewatakia  Heri huko waendako na kuwataka Watembee kifua mbele kwani wamefanya kazi kubwa Ambazo zinaonekana katika Usimamizi wa Halmashauri na Usimamizi wa Miradi ya Maendeleo.

Mkurugenzi Mtendaji Wa   Halmashauri ya wilaya ya Monduli Ndg.Stephen Ulaya amesema wamepata mafanikio makubwa na ikiwemo usimamizi mzuri katika miradi na Kusimamia pia Stahiki za Madiwani na kipindi hiki wao kama watendaji wataendelea  kusimamia yale yote yameadhimiwa katika kikao hicho  ambapo yanatakiwa kufanyiwa utekelezaji.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )